Mrembo Sofiia kutoka Ukraine
Mwanaume mmoja nchini Uingereza anayefahamika kwa jina la Tony Garnet, ameachana na mkewe aliyedumu naye kwa miaka 10 na kufanikiwa kupata watoto wawili, na kuanza mahusiano mapya na mkimbizi wa Ukraine aliyempenda ndani ya siku 10.
Tony na mkewe Lorna walijitolea kutafuta mkimbizi wa Ukraine kwa ajili ya kuishi naye nyumbani baada ya nchi hiyo kuingia katika vita dhidi ya Urusi. Katika kutafuta wakatokea kumpenda Sofiia na kuanza taratibu za kumchukua kutoka Ukraine na kumleta Uingereza.
Mwezi Mei mwaka huu Sofiia alikaribishwa ndani ya familia hiyo, na ndani ya Siku 10 baba mwenye nyumba Tony alivutiwa na binti huyo mpaka kupelekea kumuacha mkewe na kuanza maisha mapya na Sofiia.
Social Plugin