Mbunge wa Jimbo la Kongwa Job Ndugai
MBUNGE wa Jimbo la Kongwa Job Ndugai ametangaza kutogombea Ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Ndugai amesisitiza kuwa jambo la kustaafu alikwishalipanga tangu muda mrefu na kwa maamuzi hayo anaomba asitafsiriwe kuwa amestaafu kwa kushindwa.
“2025 sitagombea nafasi ya Ubunge nastaafu siyo kama nastaafu kwa kusindwa, lakini jambo ambalo tayari nilishalipanga kutoka muda mrefu uliopita hivyo tutaendelea kushirikiana kaa ambavyo tunashirikiana sasa.” alisema Ndugai.
Sakata la kustaafu kwa Ndugai limeanza tangu alipojiuzulu nafasi ya Uspika wa Bunge kufuatia sauti iliyosambaa mitandaoni ikidai nchi ikiendelea na mikopo ipo siku itauzwa kutokana na madeni.
Kutokana na kujiuzulu kwa Job Ndugai ulifanyika mchakato wa kumtafuta Spika mwingine ambapo Dkt Tulia Ackson alichaguliwa kushika nafasi hiyo mwezi Februari na Mussa Azzan Zungu kushika nafasi ya Unaibu Spika.