Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionesha Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 (Babacar Ndiaye Trophy 2022) kutokana na mafanikio kwenye Ujenzi wa Barabara, mara baada ya kukabidhiwa Tuzo hiyo na Makamu wa Rais wa Sekta Binafsi, Miundombinu na Viwanda katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Solomon Quaynor tarehe 25 Mei 2022 Accra nchini Ghana.
**
Rais Samia Suluhu Hassan, ameliandikia Bunge barua ya salamu za shukrani kuwashukuru wabunge kwa kujadili na kutoa azimio la kumpongeza baada ya kupata tuzo ya Babacar Ndiaye nchini Ghana, ambayo hupatiwa Rais wa nchi za Afrika zinazofanya vizuri kwenye miundombinu ya barabara.
Barua hiyo imesomwa leo Mei 30, 2022, na Spika wa Bunge hilo Dkt. Tulia Ackson
"Kwa kipekee kabisa tuzo hiyo ni ya wabunge kwa kutambua mchango wenu katika kusimamia miradi, matumizi sahihi ya fedha za miradi na kupitisha na kusimamia bajeti ya serikali hivyo ninaomba Watanzania wote wafurahie tuzo huku tukiendelea kusimamia, kulinda na kuitunza miundombinu yetu," imeeleza sehemu ya barua ya Rais Samia kwa Bunge.