Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PRF. HOSEA ASHINDA TENA URAIS TLS


 Na Agness Nyamaru,Arusha.

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa Chama cha Mawakili Tanganyika(TLS) Charles Rwechungura amemtangaza Prof. Edward Hosea kuwa mshindi wa nafasi ya urais katika chama hicho ambapo Prof. Hosea ameendelea kutetea kiti chake.


Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Rwechungura alimtangaza Prof. Edward Hosea kuwa mshindi kwa kuibuka na kura 621,huku Haludi Sungusia akipata kura  380 na Jeremiah  Mtobesya akipata kura 145 ikiwa jumla ya kura zilizopigwa ni  kura 1150.


Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo alimtangaza Gloria Kalabamu kuwa makamu wa rais wa chama hicho Kwa kuibuka kidedea kwa kura 598 akifuatiwa na Anjela Mbonde akipata kura 449 huku John Malya akipata kura 99 na kubainisha kuwa viongozi hao walio walioshinda wataapishwa mnamo kesho Mei 28,2022 .



Kwa upande wake Prof. Edward Hosea ambaye ni Rais wa chama hicho ameahidi kuwa na uwazi katika uongozi wake katika awamu nyingine hasa katika mahesabu yao,uwajibikaji na kuwataka wazee waliopo katika tasnia hiyo kurudi kwenye kundi ili kuweza kuwasaidia mawakili vijana waweze kufanikiwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com