Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Wadau wa Sekta ya Mawasiliano Kanda ya Ziwa katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza leo Jumanne Mei 24,2022 kilicholenga kujadili masuala mbalimbali kuhusu Sekta ya Mawasiliano . Kulia ni Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
*******
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewakutanisha wadau wa Sekta ya Mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwemo wamiliki wa vyombo vya habari vya redio, magazeti, runinga pamoja na mitandao ya kijamii kwa lengo la kujadiliana kwa pamoja namna ya kuboresha huduma za mawasiliano.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo leo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari amewahimiza wadau wa mawasiliano nchini kuchangamkia fursa za mabadiliko ya kidijitali katika kuboresha utoaji huduma.
"Nchi yetu inaenda kwenye Uchumi wa Kidijiti na unakuja na manufaa mengi hivyo tuchangamkie fursa zinazokuja na mabadiliko hayo. Panapohitaji kuwekwa sawa pawekwe haraka sana kwani biashara ya leo inaweza ikafa kesho kutokana na mabadiliko ya kidijiti", amesema Dkt. Jabiri.
Aidha Dkt. Jabiri amesema TCRA iko tayari kufanyia kazi maoni na changamoto zilizoelezwa na wadau wa mawasiliano walioshiriki kikao hicho kwa lengo la kuboresha huduma za mawasiliano nchini akisema "Tuko hapa kujadiliana na kuzungumza kwa nia ya kuboresha huduma zetu, penye mapungufu tuseme kwa lengo la kuboresha zaidi".
Naye Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo amewahimiza wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa kuwa huru na kueleza kwa uwazi namna wanavyohudumiwa na mamlaka hiyo na ikiwa kuna changamoto waziseme kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi.
Akichangia hoja kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC), Edwin Soko ameomba mamlaka hiyo kuangalia suala la gharama za usajili wa vyombo vya habari vya mtandaoni kwani bado ada ya shilingi laki tano ni kubwa na inawanyima vijana wengi fursa ya kujiajiri wanapotoka vyuoni huku wamiliki wa vyombo vya habari nao wakishindwa kuwaajiri kutokana na mazingira magumu ya uendeshaji waliyonayo.
Kwa upande wake Matrida Leopord kutoka Vision FM iliyopo Bukoba mkoani Kagera amesema Sheria ya Huduma za Vyombo Vya Habari imetatiza utendaji kazi wa waandishi wengi wa habari ambao hawakuwa na elimu kuanzia ngazi ya Diploma na kuomba sheria hiyo kuangaliwa upya.
"Sijui mlianya utafiti gani na kubaini kwamba waandishi wa haai wasio na elimu kuanzia ngazi ya Diploma hawana uwezo wa kuanya kazi. Kuna waandishi wa habati tumeshuhudia wakiwa na elimu kuanzia Diploma lakini uendaji kazi wao ado uko chini ukilinanisha na wenye Cheti", amehoji Matrida akichangia hoja kwenye mkutano huo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Wadau wa Sekta ya Mawasiliano Kanda ya Ziwa Kulia ni Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa leseni na ufuatiliaji TCRA, Thadayo Ringo. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Wadau wa Sekta ya Mawasiliano Kanda ya Ziwa Kulia ni Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo
Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Mkutano wa Mwaka wa Wadau wa Sekta ya Mawasiliano Kanda ya Ziwa
Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Mkutano wa Mwaka wa Wadau wa Sekta ya Mawasiliano Kanda ya Ziwa
Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye Mkutano wa Mwaka wa Wadau wa Sekta ya Mawasiliano Kanda ya Ziwa
Kaimu Mkurugenzi wa leseni na ufuatiliaji TCRA, Thadayo Ringo akizungumza kwenye Mkutano wa Mwaka wa Wadau wa Sekta ya Mawasiliano Kanda ya Ziwa
Social Plugin