Picha : MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI MKOA WA SHINYANGA..WAMPONGEZA RAIS SAMIA...RC MJEMA AWAPA TANO

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akifungua Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WAANDISHI wa habari mkoani Shinyanga, wamefanya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari, huku wakimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuagiza sheria kandamizi ambazo zinabinya uhuru wa habari zifanyiwe marekebisho.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Mei 16, 2022, ambayo yamehudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari, huku mgeni Rasmi akiwa Mkuu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  Sophia Mjema.

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga (Shinyanga Press Club SPC) Greyson Kakuru, akisoma hotuba kwenye maadhimisho hayo, ameomba viongozi wote wa Serikali mkoani humo, kuendelea kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari, hasa pale wanapohitaji kufanya uwiano wa habari zao (ku balance story), ili wafanye kazi kwa ufanisi na weledi mkubwa.

Pia ameiomba Serikali ya mkoa huo kutumia vyombo vya habari kutangaza fursa zilizopo, pamoja na mazuri ambayo yametekelezwa na Serikali, na siyo kusubiri hadi ziara za viongozi wakubwa, ili kuutangaza mkoa na kupata wawekezaji, na wananchi kufahamu miradi ya maendeleo ambayo wametekelezewa.

"Tunaomba viongozi wa Serikali kuweka utaratibu wa kila mwaka, kutumia vyombo vya habari kutangaza miradi ya Serikali ambayo imetekeleza, na siyo kusubiri hadi ziara za viongozi kitaifa au wa mikoa na wilaya," amesema Kakuru.

Aidha, ameupongeza pia mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) kwa kufadhili Klabu hiyo ya waandishi wa habari na kutekeleza mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga, na kutekeleza mpango mkakati wa kitaifa wa Serikali MTAKUWWA wa kutokomeza ukatili wa wanawake na watoto.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mstaafu wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga Kadama Malunde, ambaye ni Mkurugenzi wa Malunde 1 blog akiwasilisha mada ya Mitandao ya Kijamii na Uandishi wa Habari na changamoto za kidigiti, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan,kwa kuelekeza sheria kandamizi ambazo zina binya uhuru wa habari zifanyiwe marekebisho kwa kushirikisha wadau wote wa habari.

"Tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan tangu ameingia madarakani tumeona mabadiliko chanya ya ukuaji sekta ya habari hapa nchini"amesema Malunde.

"Kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Jijini Arusha,Mei 3,2022 Rais Samia alisema ameshamuelekeza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari Nape Nnauye, kuwa Sheria za habari ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kubinya uhuru wa habari zifanyiwe marekebisho na kushirikisha wadau wote, tunampongeza kwa hilo,"ameongeza Malunde.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amewapongeza wanahabari mkoani humo kwa kazi zao nzuri ambazo wanazifanya, huku akiahidi kuwapatia ushirikiano, na pale wanapokumbana na changamoto wasisite kumweleza ili zitafutiwe ufumbuzi.

“Sijawahi kupata tatizo na waandishi wa haabari wa mkoa wa Shinyanga, wanafanya kazi vizuri, wanafanya kazi kwa weledi. Nimeona wana uweledi, wana balance story, naomba tuendelee kushirikiana. Tunawashukuru waandishi wa habari kwa kuendelea kushirikiana na serikali, endeeleni kuripoti mambo mazuri yanayofanywa na serikali”,amesema Mjema.

Amewataka waandishi hao wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao, wazingatie suala la weledi, maadili ya taaluma, taratibu za nchi, maelekezo ya Serikali, pamoja na kuandika habari za uwiano wa pande zote mbili.

Mjema amewaasa pia wanahabari hao kutumia kalamu zao vizuri kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye zoezi la kuhesabiwa sensa ya watu na makazi ambalo litafanyika Agosti 23 mwaka huu nchini kote.

Ametumia pia fursa hiyo kutoa wito kwa wazazi mkoani humo kuwapeleka watoto wao wakapate Chanjo ya Polio zoezi ambalo litafanyika kuanzia Mei 18 hadi 21 mwaka huu, ili watoto wapate kinga dhidi ya ugonjwa huo wa kupooza.

Aidha, maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari hufanyika kila mwaka Mei 3,ambapo kimkoa mkoani Shinyanga yamefanyika leo Mei 16, huku kitaifa yakifanyika Jijini Arusha na mgeni Rasmi alikuwa Rais Samia Suluhu Hassan, yenye kauli mbiu isemayo uandishi wa habari na changamoto za kidigiti.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akifungua Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga. Picha na Kadama Malunde & Marco Maduhu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akifungua Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru akisoma hotuba kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru akisoma hotuba kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru akisoma hotuba kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga
Wadau wa habari wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga
Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde akiwasilisha mada kuhusu Mitandao ya Kijamii na Uandishi wa Habari na Changamoto za Kidigiti kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga

Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde akiwasilisha mada kuhusu Mitandao ya Kijamii na Uandishi wa Habari na Changamoto za Kidigiti kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Mwanza, Edwin Soko akiwasilisha mada kuhusu Usalama Mtandaoni na umuhimu wa Klabu za waandishi wa habari na wadau katika maendeleo ya mikoa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga

Mkurugenzi wa Radio Faraja Padre Anatoly Salawa akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga
Katibu wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Ali Lityawi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga

Mjumbe wa kamati Tendaji SPC, Michael Mipawa akitoa neno la shukrani kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga
Mwandishi wa Habari Stephen Wang'anyi akiwashukuru wadau na waandishi wa habari waliomsaidia kipindi chote tangu alivyopata ajali ya pikipiki mwaka 2019 na sasa anaweza walau kutembea japo hawezi kufanya kazi yoyote leo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga

Mfanyabiashara maarufu wa nguo Neema Chacha 'Ney Fashion' akichangia hoja kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga
Mtafiti wa mila za Kabila la Wasukuma, Sonda Kabeshi akichangia hoja kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Mei 16,2022 katika ukumbi wa Witeshi Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post