Mganga wa kienyeji
Na Walter Mguluchuma - Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia mganga wa kienyeji aitwaye Akili Abakuki ( JIMMY) (38) Mkazi wa Majengo Manispaa ya Mpanda kwa tuhuma za kuwalawiti watoto sita mida ya usiku wakati alipokuwa akiwapatia matibabu ya tiba za kienyeji.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Sylivester Ibrahim amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa hapo Mei nane majira ya saa saba mchana huko katika eneo la Hospitali ya Mkoa wa Katavi iliyoko katika Kata ya Kawajense Manispaa ya Mpanda .
Amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya mama mmoja mkazi wa Mtaa wa Makanyagio alipogundua mtoto wake wa miaka 10 wanafunzi wa darasa la tatu jina limehifadhiwa aliyekuwa amempeleka kwa mganga huyo kupatiwa matibabu ya uganga wa kienyeji kuwa amelawatiwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi alisema baada ya kupatikana taarifa hizo jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo ambaye pia alikuwa amewalawiti watoto wengine watano wakati akiwafanyia matibabu ya tiba za kienyeji wenye umri kati ya sita na miaka 12.
Amebainisha kuwa wazazi wa watoto hao walikuwa wakiwapeleka watoto wao kwa mganga huyo kwa ajiri ya kupatiwa tiba za kienyeji ambapo katika tiba hizo Mganga huyo alikuwa akitoa masharti kuwa tiba zake ni lazima azitowe usiku hivyo ni lazima watoto hao walale kwake bila wazazi wao kuwepo .
Ilipokuwa ikifikia usiku mganga huyo alikuwa anawadanganya kwa kuwapatia zawadi ndogo ndogo kama pipi biskuti na jojo na kisha anawavua nguo na kuwapaka mafuta mwili mzima na kuwalawiti .
Kaimu Kamanda Sylivester Ibrahim alisema vitendo hivyo vya kuwalawiti watoto hao alikuwa akivifanya ndani ya chumba chake alichokuwa akiishi usiku wa manane huku akiwatishia watoto hao wasiwaambie wazazi wao kama amewafanyia kitendo hicho .
Aidha Kaimu Kamanda amewahimiza wazazi Mkoani Katavi kufuatilia vitendo ambavyo wanaweza kuwa wamefanyiwa watoto wao na pia wazazi waache tabia ya kuamini imani potofu na za kishirikina .
Social Plugin