MWANZA PRESS CLUB YAKARIBISHA WADAU WA HABARI KUSHIRIKI
Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa Mwanza (Mwanza Press Club - MPC) inazialika taasisi za serikali, taasisi zisizo za serikali, sekta binafasi na mdau mmoja mmoja wa habari kutoka Kanda ya Ziwa kushiriki sherehe maalum (usiku wa marafiki wa vyombo vya habari) Kanda ya Ziwa.
Sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika Mei 27, 2022, katika ukumbi wa Hotel ya Gold Crest Jijini Mwanza.
Lengo la usiku wa wadau
Mosi; kuwaleta pamoja wadau wa habari ili waweze kueleza tathmini yao ya mwaka mmoja wa utekelezaji wa mipango yao ya mwaka ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Pili; kuwapa wadau wa habari nafasi ya kuonyesha bidhaa au huduma zao mbele ya vyombo vya habari ili kuzitangaza kwa kuziandikia habari ili jamii iweze kuzijua.
Tatu; kujenga mahusiano ya kikazi baina ya vyombo vya habari na wadau wa habari.
Faida ya udhamini wa usiku wa marafiki wa habari
1. Kuhudhuria mkutano wa vyombo vya habari wa awali/ press conference ambapo kila mdau atapata nafasi ya kuzungumzia taasisi yake.
2. Kuweka logo ya taasisi husika Tshirt na mabango.
3. Mabanda ya maonyesho kwa wadau kuonyesha huduma au bidhaa zinazozalishwa au kutolewa na mdau.
4. Nafasi itatolewa siku ya tukio kwa kila mdau kueleza shughuli za taasisi yake.
5. Mabango (bannners) za Taasisi zitawekwa ukumbini.
6. Makala maalumu na habari za wadau zitapata nafasi kwenye vyombo mbalimbali vya habari zikiwamo Tv, online tv, Redio, Blogs na Magazeti ya Kiswahili na Kiingereza.
Namna ya kushiriki
Taasisi yoyote ya serikali na isiyo ya serikali ama mtu binafsi yeyote akitaka kushiriki wasiliana nasi kupitia namba zifuatazo.
0754 551306
0629436495
Wageni waalikwa ni pamoja na;
1. Mawaziri wa Wizara mbalimbali
2. Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa
3. Wakuu wa taasisi za serikali na zisizo na kiserikali.
4.Wamiliki wa vyombo vya habari.
5. Wahariri wa vyombo vya habari.
6. Waandishi wa habari.
WOTE MNAKARIBISHWA
Social Plugin