Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : WAUGUZI HOSPITALI YA MANISPAA YA KAHAMA WAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI


Wauguzi wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama wakicheza muziki wakati wa sherehe yao ya Wauguzi Duniani Mei 27,2022. Picha na Patrick Mabula
Wauuguzi wa hospitali ya Manispaa ya Kahama wakiwa kwenye maadamano wakati wa sherehe ya Wauuguzi Duniani iliyofanyika katika viwanja vya jengo jipya la wagonjwa wa nje ,OPD.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Wauguzi wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama Dk.Shani Josephat kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akitoa hutuba yake kwenye sherehe ya siku ya Wauguzi Duniani Mei 27,2022
Muuguzi mkuu wa hospitali ya Manispaa ya Kahama , Luja Jimila akisoma taarifa yake katika maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani.
Muuguzi Milembe Makonge akisoma risala ya Wauguzi wa Manispaa ya Kahama kwenye maadhimisho ya sherehe yao ya siku ya Wauuguzi Duniani
Jengo jipya la hospitali ya Manispaa ya Kahama baada ya kuanza kufanyakazi hivi karibuni. Na Patrick Mabula - Kahama.



Wauguzi wa hospitali ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wameungana na wauguzi wenzao duniani kuadhimisha siku ya wauguzi duniani kwa kufanya kazi mbalimbali ikiwemo kuhamasisha wananchi kuchangia damu na kufanikiwa kukusanya uniti 97, kutoa mafunzo ya taaluma ya uuguzi, kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi, elimu ya lishe kwa akina mama wenye watoto wachanga na watu wazima na uchunguzi wa magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza.


Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Mgeni rasmi ,Mganga mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama Dkt. Shani Josephat, kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga amewapongeza wauuguzi hao kwa kufanya kazi kwa moyo wa kujituma na kuwataka waendelee kuwa na nidhamu , utii na kuzingatia maadili ya kazi wakati changamoto zao zinapofanyiwa kazi na serikali.

Muuguzi mkuu wa hospitali ya Manispaa ya Kahama Luja Jamila amesema wauguzi wamekuwa wakifanya kazi nyingi na kutaka waendeelee kuheshimiwa kutokana na wajibu wao wa kazi wa kuhudumia wagonjwa na pengine kufanya kazi za madaktari.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com