Mtu aliyeuawa na wananchi
**
Mtu mmoja mkazi wa Sojema, Kata ya Murieti Jijini Arusha, ameuawa na wananchi baada ya kukamatwa katika nyumba ya moja ya wakazi wa eneo hilo akijaribu kufanya uhalifu, huku wengi wakimhusisha na mtu ajulikanae kama 'Teleza' anayetuhumiwa kuwaingilia wanawake kinguvu hasa nyakati za usiku.
Mtu huyo ambaye haikuwa rahisi jina lake kujulikana kwa haraka, amekutwa na mauti hayo majira ya saa 10:00 alfajiri baada ya kukurupushwa na baadhi ya wakazi wa Murieti kwa kushirikiana na vijana wa sungusungu ambao kwa muda wamekuwa wakishika doria katika kipindi hiki cha habari za teleza kuzagaa katika eneo lao.
Akizungumza Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo, amethibitisha kushambuliwa kwa mtu huyo na kutoa rai kwa wananchi kutojichukulia sheria mkononi kwani hupunguza wigo wa upelelezi wao.
Chanzo- EATV
Social Plugin