000
Katibu mkuu wa taasisi ya utaalamu na utawala Tanzania (APAT) Mhe.Christopher Kabalika akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa mkutano wao wa kimataifa wenye lengo la kujadili mustakabali wa kuunganisha vyama vya utawala na vyama vya rasilimali watu na kuwakutanisha maafisa rasilimali watu na wataalamu zaidi ya 500 mkoani Arusha.
**************
Na Agness Nyamaru, Arusha.
Taasisi ya utaalamu wa utawala Tanzania(APAT) imewakutanisha maafisa rasilimali watu na watawala zaidi ya 500 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania mkoani Arusha katika mkutano wao wa kimataifa wenye lengo la kujadili mustakabali wa kuunganisha vyama vya watawala na vyama vya rasilimali watu ili kuona namna ya kuunda bodi itayokuwa inasimamia masuala ya pande zote mbili.
Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano wao ulioanza May 18, 2022 katibu mkuu wa taasisi hiyo Mhe. Christopher Kabalika alisema kuwa wanataka wawe na chama kimoja kikubwa, chenye nguvu ambacho kitaweza kubeba maana ya watawala na rasilimali watu kujua nini kinafanyika katika taifa.
“Lakini pia tutajadili namna gani tutaweza kuunda bodi ya maafisa rasilimali watu na watawala Tanzania ili mambo yetu yote yaweze kupitia kwenye bodi hiyo kwaajili ya kudhibidi na kujua nini tutafanya kama ilivyo katika bodi zingine zinazosimamia taaluma mbalimbali,”Alisema Mhe.Kabalika.
Alifafanua kuwa mkutano huo ni wa siku tatu ambapo watajadili agenda mbalimbali na siku ya mwisho wanatarajia utafungwa na waziri wa utumishi na utawala bora Jenista Muhagama ambapo wameiomba serikali kuangalia kiumakini iwe weweze kupata bodi.
Kwa upande wake Afisa utumishi manispaa ya temeke Bihaga Yogwa alieleza kuwa bado kuna changamoto ya kutokuwa na bodi katika tasnia hiyo kwani wanakosa chombo kimoja kinachosimamia mambo yao lakini wakipata bodi watakuwa imara na wenye nguvu zaidi katika kushughulika na masuala yao.
Naye muhadhiri kutoka chuo kikuu cha Mzumbe Dkt Venance Shillingi alisema kuwa watakapo unganisha kada hizo mbili itawafanya wawe na nguvu itakayoshawishi serikali na bodi ya kuwasimamia kwani wakiwa na bodi hiyo kada hizo zitakuwa vyema na ndipo aweze kuwa afisa utumishi au afisa utawala.
“Kazi ya afisa utumishi sio kuajiri tu na kufukuza bali ni mtu pekee ambaye anaweza kufanya taasisi ikafanya vizuri kuliko kada nyingine yoyote na hii itafanya afisa utumishi wawe ni sehemu ya taasisi kwa kujua zina mikakati gani kwa miaka ijayo ili waweze kusaidia kupata wenye sifa stahiki ya kutekeleza hiyo mikakati,”Alisema Dkt Shillingi.
Alisema kuwa wakishaunganisha nguvu na kitu kimoja watakuwa na matawi mawili moja la maafisa utumishi na lingene utawala lakini kwaujumla wanakuwa timu moja ili watakapokuwa na hoja yoyote waweze kusikilizwa.
Social Plugin