Mwili wa mtu aliyedhaniwa kufariki na kupelekwa Mochwari ukirudishwa baada ya kugundulika kuwa yupo hai
**
RAIA mmoja katika Jiji la Shanghai nchini China amepelekwa mochwari kwa bahati mbaya akidhaniwa ni maiti kumbe bado yupo hai.
Katika Jiji ambalo limeshmbuliwa na tatizo kubwa la Uviko -19, limetokea tukio hilo la kustua ambapo mwili wa mzee mmoja mkazi wa jiji la Shaghai uliwekwa katika begi maalum la kuhifadhia maiti na kupelekwa mochwari ambapo mhudumu wa Mochwari aligundua kuwa mtu alikuwa hajafa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Utangazaji la CNN ni kwamba picha za video za tukio hilo zilichukuliwa na Jirani ambaye alikuwa ghorofani huku akipaza sauti akisema manesi wanamchukua mtu aliyehai na kumpeleka mochwari.
Madaktari wa zamu wakifuatilia sakata la mtu ambaye alipelekwa mochwari akiwa hai
Serikali ya Shanghai tayari imechukua hatua kuhusu tukio hilo ambapo kwanza imethibitisha kuwa hali ya mtu hiyo kwa sasa imeimarika lakini tayari imemnyang’anya Cheti Daktari aliyehusika katika Sakata hilo ambaye pia yupo chini ya uchunguzi, Maafisa watatu wa afya wameshaondolewa katika nafasi zao lakini pia Mkuu wa Idara ya Uuguzi naye ameondolewa katika nafasi yake.
Tayari kumekuwa na mtazamo mbalimbali kutoka kwa wananchi wa China na wengi wao wameonesha kukerwa huku wakiishutumu Serikali kutokuwa makini na Maisha ya raia hasa wa Jiji la Shanghai ambako mamilioni ya wakazi wamepigwa Lock Down.
Kupitia mtandao maarufu wa kijamii unaofanana na Twitter huko nchini China wa Weibo mmoja wa raia wa Shanghai amesema:
Gari la wagonjwa ambalo limebeba mwili wa mtu aliyedhaniwa kufariki
“Hili linaonekana kama tukio la mauaji ya kudhamiria.”
Nchi ya China hasa katika Jiji la Shanghai inakabiliwa na tatizo kubwa sana la Uviko-19 kiasi kwamba kume kuwa na Lock Down ambayo imeathiri mamilioni ya wtu katika Jiji hilo.
Social Plugin