Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, akiongea katika mkutano na wadau wa habari Arusha Mei 5, 2022, ambao imeandaliwa na MISA-Tanzania na TAMWA kwa ufadhili wa International Media Support (IMS).
Mwenyekiti wa MISA-Tanzania, Salome Kitomari, akiongea katika mkutano na wadau wa habari na serikali jijini Arusha Mei 5, 2022, ambao umeandaliwa na MISA-Tanzania na TAMWA kwa ufadhili wa International Media Support (IMS)
Mwenyekiti wa TAMWA, Joyce Shebe, akiongea katika mkutano na wadau wa habari na serikali jijini Arusha Mei 5, 2022, ambao umeandaliwa na MISA-Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA kupitia ufadhili wa International Media Support (IMS)
(Kutoka kushoto) Meneja Programu wa International Media Support (IMS), Fausta Musokwa, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, Mkurugenzi wa Tanzania Media Fund, Dastan Kamanzi, wakishiriki kwenye mkutano na wadau wa habari na serikali jijini Arusha Mei 5, 2022, ambao umeandaliwa na MISA-Tanzania na TAMWA kwa ufadhili wa IMS
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wadau wa habari na serikali jijini Arusha Mei 5, 2022, wakifuatilia mada kutoka kwa wazungumzaji. Mkutano huo umeandaliwa na MISA-Tanzania na TAMWA kwa ufadhili wa International Media Support (IMS)
**
TAASISI ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Kusini (MISA-Tanzania) kwa kushirikiana na Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) imeandaa mkutano leo Mei 5, 2022, kati ya wadau wa vyombo vya habari na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Zaidi ya washiriki 50 kutoka taasisi mbalimbali za vyombo vya habari na sheria nchini Tanzania wanashiriki mkutano huo kwenye hoteli ya Four Points by Sheraton leo Alhamisi Mei 5,2022.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amemuwakilisha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, pamoja na timu yake amehudhuria mkutano huo wa siku moja uliofadhiliwa na taasisi ya International Media Support (IMS).
Wakifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa MISA-Tanzania, Salome Kitomari, na Mwenyekiti wa TAMWA, Joyce Shebe, wamesisitiza umuhimu wa mahusiano mazuri kati ya serikali na vyombo vya habari nchini.
Naye Msemaji Mkuu wa Serikali , Gerson Msigwa aliwataka waandishi kuheshimu maadili na kuepuka "tug-of-war" au mvutano na serikali.
Mkutano huu unakuja siku moja baada ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani iliyohudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan hapa jijini Arusha.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni Uandishi wa Habari na Changamoto za Kidijiti.
Mashauriano kati ya wadau wa vyombo vya habari na serikali ni sehemu ya kutafuta maridhiano ya kurekebisha sheria kadhaa kandamizi zinazoathiri uhuru wa vyombo vya habari nchini, ikiwemo Sheria ya Huduma ya Habari, 2016.
Social Plugin