WAZIRI MKENDA : SERIKALI IMEDHAMIRIA KUWEKEZA ZAIDI KWENYE ELIMU NA UTAFITI WA TIBA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Afolf Mkenda akizungumza leo 14 Mei 2022 wakati wa siku ya maadhimisho ya ugonjwa wa LUPUS TANZANIA iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Jijini Dar es salaam.


Na Mathias Canal, Dar es salaam


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Afolf Mkenda amesema kuwa serikali imedhamiria kuwekeza zaidi kwenye elimu ya utafiti na tiba.


Huo ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 na mpango mkakati wa serikali kupitia bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mwaka 2022/2023 ambapo imepanga kutoa motisha kwa wahadhiri kutoka chuo chochote cha serikali ama binafsi akiweza kuchapisha andiko lake kwenye majarida ya juu, serikali itampa Shilingi milioni hamsini.


Waziri Mkenda ameyasema hayo tarehe 14 Mei 2022 wakati wa siku ya maadhimisho ya ugonjwa wa LUPUS TANZANIA iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Jijini Dar es salaam.


Waziri Mkenda mesema kuwa kwa jumla yake serikali imetenga Bilioni moja kwa ajili ya wahadhiri hao na kufanya hivyo serikali inalenga kujenga uhusiano na uwezo zaidi kwa watafiti ili kuimarisha kipato chao jambo litakalowafanya waweze kufanya utafiti wakati wote na kwa ufanisi mkubwa zaidi.


Amesema kuwa serikali itawawezesha wanafunzi wote ikiwemo kuwasomesha katika vyuo vikuu kwa wale watakaofaulu kwa kiwango cha juu kwenye masomo ya Sayansi.


Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof Andrea Pembe amesema kuwa serikali imeweka kipaumbele kwenye magonjwa mbalimbali ikiwemo uraibu wa madawa ya kulevya na magonjwa ya kina mama yatokanayo na ujauzito hivyo kuwepo kwa huduma hiyo nchini kumerahisisha kuwahudumia wananchi kwa kuwapatia tiba kirahisi wagonjwa ikiwa ni pamoja na upatikanaji kwa urahisi wa dawa japo gharama za dawa bado ni kubwa sana.


Prof. Pembe amesema kuwa katika tafiti zilizofanyika kwenye ugonjwa wa Lupus zinaonyesha watu wa asili ya Afrika ndio waathirika wakubwa na inakadiriwa watu 70-100 wanaathirika na ugonjwa wa Lupus kati ya watu 100,000.

Waziri Mkenda ameongeza kuwa wanawake ndio wanaathirika zaidi na ugonjwa huo kwa uwiano wa wanawake 10 kwa mwanaume mmoja.


Aidha katika utafiti uliofanyika katika hospitali ya Taifa kutambua watoto waliokuwa na magonjwa rheumatism kwa kipindi cha miaka 7 (2012-2019) ulitambua watoto 52 waliokuwa na hayo magonjwa na miongoni mwao watoo 8 ambao ni sawa na asilimia 15% walikuwana ugonjwa wa Lupus.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Afolf Mkenda akizungumza leo 14 Mei 2022 wakati wa siku ya maadhimisho ya ugonjwa wa LUPUS TANZANIA iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Jijini Dar es salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post