SpikaMahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imeridhia wabunge 19 wa viti maalum waliovuliwa uanachama wao na CHADEMA kuendelea na ubunge wao mpaka maombi ya kibali cha kufungua kesi ya kupinga uamuzi wa kamati kuu ya CHADEMA ulioridhiwa na wajumbe wa baraza kuu utakaposikilizwa na kutokewa uamuzi.
Maombi hayo ya zuio la muda la ubunge wao, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), yamesikilizwa leo Jumatatu, Mei 16, 2022 mbele ya Jaji John Mgetta.
Mnamo Mei 12, 2022, Baraza Kuu la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA lilitoa uamuzi wa kuwafuta Uanachama Wabunge hao 19.
Jambo hilo lilipelekea mapema leo Mei 16, 2022 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson kutolea maelezo na ufafanuzi juu ya sakata la wabunge hao, ambapo alisema jambo hilo lipo mahakamani na Mahakama ndiyo chombo pekee kinachoweza kutoa haki.