Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAANDISHI WA HABARI KIGOMA WAADHIMISHA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI...RC ANDENGENYE ATAKA VIONGOZI, WADAU KUSHIRIKIANA NA WANAHABARI


Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye akizungumza katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari kwa mkoa Kigoma yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Social mjini Kigoma.
Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye akizungumza katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari kwa mkoa Kigoma yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Social mjini Kigoma.
Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye akizungumza katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari kwa mkoa Kigoma yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Social mjini Kigoma.
Wadau wa habari mkoani Kigoma
Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa Kigoma Deogratius Nsokolo akizungumza katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari iliyofanyika kimkoa mjini Kigoma.
Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa Kigoma Deogratius Nsokolo akizungumza katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari iliyofanyika kimkoa mjini Kigoma.
Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

MKUU wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye ametoa wito kwa viongozi na wadau wa habari mkoani humo kushirikiana na waandishi wa habari na kuwapa nafasi kufanya kazi zao kwa uhuru badala ya kuwaweka mfukoni na kuandika mambo ambayo viongozi hao hao wanataka.

 

Andengenye alisema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari ambayo kimkoa yamefanyika leo na kusema kuwa ni jambo baya kujenga urafiki ambao utawafanya waandishi wa habari kuandika mambo kwa uhuru na badala yake kuandika mambo ambayo yatawafurahisha viongozi.

 

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa ni vizuri vyombo vya habari vikaandika habari kwa uhuru kwa maana ya kukosoa, kuelimisha na kuuitaarifu jamii mambo yanayotokea lakini jambo hilo linapaswa kufanywa kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari na taratibi zinazoongoza sheria na taratibu za nchi.

 

“Kuwa Mwandishi wa habari haikuoi nafasi ya kuandika kila kitu unachojisikia hata kama mengine siyo ya kweli, nan i vizuri waandishi wa habari wakawapa nafasi viongozi na wadau wao kujibu na kutoa maelezo na ufafanuzi mambo mbalimbali badala ya kuandika habari za upande mmoja ambazo nyingine zinazua taharuki kwenye jamii,”Alisema Mkuu huyo wa mkoa.

 

Pamoja na hivyo alisema kuwa mkoa Kigoma unafunguka kwenye suala zima la masuala ya uchumi hivyo ni vizuri vyombo vya habari vikatumika kutangaza rasilimali za mkoa na viongozo wa serikali, taasisi za umma na wadau wa habari wanapaswa kutoa taarifa bila kificho waka hila na jambo hilo lifanywe kwa kufuata itifaki ya wasemaji rasmi waliopewa mamlaka ya kufanya hivyo.

 

“Tunaposema waandishi wa habari wapewe uhuru hatusemia wafanye kila kitu ni lazima itifaki zifuatwe hasa kwa wasemaji wanapaswa kutoa taarifa na ufafanuzi siyo kila mmoja anaweza kuwa msemaji wa jambo na kufuata itifaki itasaidia kuondoa changmoto ya waandishi wa habari kulalamika kunyimwa ushirikiano,,”Alisema Andengenye Mkuu wa mkoa Kigoma.

 

Mkuu huyo wa mkoa ametoa wito kwa Waandishi kufuata  sheria na taratibu za nchi ili kuepuka kuingia kwenye migogoro ya uvunjifu wa sheria na kuipaka matope tasnia sambamba na kuwataka kujielemisha na kuongeza elimu zao

 

Awali Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa Kigoma,Deogratius Nsokolo alisema kuwa maadhimisho hayo yanalenga kuwaweka pamoja waandishi wa habari na wadau ili kujadili changamoto zinazojitokeza katika utendaji wa kila siku wa vyombo vya habari, waandishi wa habari na utoaji habari kwa viongozi na wadau.

“MKutano huu unajadili hali iliyopo sasa na hatua za kuchukua na jambo hili linafanywa kwa pamoja baina ya waandishi wa habari na wadau wetu ambao ndiyo wanaotoa habari ili ziweze kwenda kwa wananchi ambao sisi sote ndiyo tunaowatumikia,”Alisema Mwenyekiti huyo wa Press Club.

Aidha Mwenyekiti huyo alitumia nafasi hiyo kumuomba Mkuu wa mkoa Kigoma kuweka mazingira ambayo yatawafanya wadau wa habari hasa wa taasisi za serikali ambao wakati mwingine wana jambo linalopaswa kupatiwa ufafanuzi lakini wamekuwa hawatoi ushirikiano.

Kauli Mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni uandishi wa habari na changamoto ya kidijitali ambayo inaeleza mabadiliko ya kiteknolojia na namna waandishi wa habari wanavyofanya kazi zao lakini pia kuwepo kwa changamoto zinazosababishwa na maendeleo ya kidijitali duniani.

Mwenyekiti huyo wa Kigoma Press Club  alisema kuwa kumekuwa na ushirikiano mkubwa kwa wadau mbalimbali ingawa kumekuwa na changamoto ambazo zimejitokeza kwa baadhi ya wadau lakini kumekuwa na vikao mbalimbali ambavyo vimekuwa vikikabiliana na hali hiyo.

Mmoja wa wadau wa habari waliohudhuria maadhimisho hayo Mratibu wa miradi wa shirika la Nyakitonto Youth Delepment, Ramadhani Joel alitoa pongezi kwa kazi kubwa inayofanywa na waandishi wa habari mkoa Kigoma lakini bado zipo changamoto za kuwepo kwa habari kwa baadhi ya matukio.

Ramadhani alisema kuwa waandishi wa habari wanapaswa kwenda sambamba na mabadiliko ya kiteknolojia kwa kuandika habari za uchunguzi hasa wananchi vijijini sambamba na kufanya habari za uchunguzi wakitafuta miradi kwenye taasisi mbalimbali kwa ajili ya kufanya kazi hizo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com