Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SHIRIKALA THUBUTU AFRICA LAZINDUA MRADI WA HISANI KATIKA JAMII


Viongozi mbalimbali wa kata zilizolengwa na mradi huo wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa mradi wa Hisani katika jamii( Community Philanthropy)

Na Suzy Luhende,Shinyanga
Shirika lisilo la kiserikali la Thubutu Africa Initiatives (TAI) limezindua mradi wa Hisani katika jamii( Community Philanthropy) kwa ajili ya kuhamasisha jamii ya manispaa ya Shinyanga kuweza kutumia rasilimali zao katika kutatua baadhi ya changamoto zao bila kusubili fedha za serikali na wadau wengine.


Mradi huo umezinduliwa leo Mei 20,2022 mjini Shinyanga na katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga aliyewakilishwa na Chila Moses ambaye ni afisa Mipango na uratibu kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, ambaye amesema ni jambo zuri kuwepo kwa mradi huo, kwa kuwa unaleta mbinu ya moja kwa moja ya kutatua matatizo ya jamii husika zinazo wazunguka.


"Ninawaomba wote tuliopo hapa tukawahamasishe wananchi ili waweze kujitolea na kuweza kufanikisha mradi huu kwani mpango huu ni mzuri wa kuleta maendeleo na kuondoa changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii",amesema Chila.


Mkurugenzi wa shirika la Thubutu Africa Initiatives Jonathan Manyama amesema ni jambo la kawaida limezoeleka la utoaji kuhusu maendeleo ya wengine ila ni wakati wa jamii yenyewe kutatua changamoto zao kwa kutumia rasilimali walizonazo katika maeneo yao.


" Mfumo huu umefanikiwa na kwa nchi za wenzetu kwa kiwango kikubwa kwa jamii yenyewe kutatua matatizo yao bila kusubili nguvu ya serikali na wahisani wa maendeleo,ni wakati wa kubadili tabia za jamii yetu ili iweze kujitoa zaidi kwa rasilimali zao kusaidia maendeleo binafsi kwa kuwashirikisha wenyewe", amesema Jonathan.


"Mradi huu utafanyika katika manispaa ya Shinyanga na utalenga kata nne ambazo ni kata ya Lubaga, Old Shinyanga, kata Mwamalili, kata ya Mjini, ambapo kata ya Lubaga tunatarajia kujenga choo cha watoto wa kike katika shule ya msingi Lubaga"amesema Manyama.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la TVMC Mussa Ngangala ambaye pia ni mjumbe baraza la NGO Taifa (NACONGO) amesema yeye binafsi alishawahi kujitolea kuondoa changamoto kivuko mtaa wa kitangili,lakini aliambiwa ni kihelele na wananchi,lakini baada ya kufanikisha kuondoa tatizo hilo alianza kusikia maneno kuwa huyu kijana anajitahidi kufanya maendeleo ya mtaa wetu.


Diwani wa kata ya Lubaga ,Reuben Dotto amesema ametiwa moyo kwa mradi huo kuanza kutekelezwa katika kata ya Lubaga na atahakikisha anakamilisha matundu ya vyoo katika shule ya sekondari kata ya Lubaga bila kusubili fedha za serikali bali kutumia ushirikishwaji wa wananchi wenyewe.


Afisa maendeleo ya Jamii Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga John Tesha amesema serikali haiwezi kufanya kila kitu ili kuondoa changamoto mbalimbali ndani ya jamii, bali yapo yanayowezekana kwa wanajamii wenye bila kusubili serikali, hivyo wananchi wakishirikishwa wanaweza kujitoa kwa ajili ya maendeleo, hata kwenye harusi jamii inajitoa haiwezi ikashindwa kwenye suala la kimaendeleo.

Afisa maendeleo wa mkoa wa Shinyanga 
Tedson Ngwale amesema suala hili ni jambo la msingi, kwani rasilimali kubwa ni wananchi, hivyo nguvu ya wananchi inaaminika wakitaarifiwa tu kuna changamoto ya kitu furani watatoa ushirikiano na mradi huu umepokelewa na mkoa kwa sababu serikali inaamini nguvu ya wananchi


Katika uzinduzi huo pia ulifanyika uchaguzi wa kamati ya jamii ya wanashinyanga ya kusimamia mradi huo ambayo itasimamiwa na mwenyekiti aliyechaguliwa Joseph Ndatala ambaye amesema atafanya kazi kwa uaminifu na kamati yake ili kuhakikisha mradi huo unafanikiwa.
Mgeni rasmi Chila Moses ambaye ni afisa Mipango na uratibu kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, aliyemwakilisha katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary wakati wa uzinduzi wa mradi wa Hisani katika jamii( Community Philanthropy)
Afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi wa Hisani katika jamii( community Philanthropy).
 Mkurugenzi wa shirika la TAI Jonathan Manyama akitoa maelekezo juu ya mradi huo.
 Mkurugenzi wa shirika la TAI Jonathan Manyama akitoa maelekezo juu ya mradi huo.
 
Afisa maendeleo wa manispaa ya Shinyanga John Tesha akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo.
Afisa maendeleo wa manispaa ya Shinyanga John Tesha akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo.
Afisa Mradi kutoka shirika la TAI. Paschalia Mbuguni akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo
Wajumbe wa kamati ya kusimamia kamati ya kusimamia mradi wa Hisani katika jamii wakiwa kwenye picha ya pamoja
Mwenyekiti wa kamati ya kusimamia mradi wa Hisani katika jamii Joseph Ndatala akizungumza baada ya kuchaguliwa.
Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Mussa Jonas Ngangala akichangia hoja juu ya mradi huo
Diwani wa kata ya Lubaga Reuben Dotto akichangia hoja kwenye uzinduzi wa mradi huo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com