MWANAMKE AUAWA KWA KUCHOMWA KISU GESTI MJINI KAHAMA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando

Na Marco Mipawa - Kahama

Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Zuena au Ashura Salum (25-30) mkazi wa Dar es Salaam, amekutwa chumbani akiwa ameuawa kwa kuchomwa kisu  na mtu anayedhaniwa kuwa ni mwenza wake katika nyumba ya kulala wageni ya Kalunde iliyoko mjini Kahama, usiku wa kuamkia Mei 22, 2022.


Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga George Kyando amethibitisha kutokea kwa  tukio hilo na kwamba, Zuena na mwanaume huyo waliingia chumbani hapo majira ya saa 11:00 alfajiri na kwamba mwanaume alitoka na kutokomea kusikojulikana kabla ya wahudumu wa nyumba hiyo kugundua mauaji hayo.


Kyando amesema, mapema asubuhi siku hiyo wahudumu wa nyumba hiyo waliukuta Mwili wa marehemu chumbani pamoja na simu mbili zenye laini zinaonesha majina hayo.

Amesema jeshi la polisi linaendelea kufuatilia tukio hilo, huku akitoa Rai kwa jamii kujihadhari na watu wasiotambulika vizuri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم