Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BRELA YAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI MJINI MOROGORO



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara ,Dkt.Hashil Abdallah akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili kati ya wahariri wa vyombo vya habari na BRELA kinachoendelea leo mkoani Morogoro.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni, Bw.Godfrey Nyaisa akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah katika kikao kazi hicho.


Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw. Deodatus Balile akitoa shukurani zake kutoka (TEF)kwa Naibu Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni, Bw.Godfrey Nyaisa mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi hicho.



Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano BRELA Bo Roida Andusamile akitoa ratiba ya mawasilisho mbalimbali yatakayotolewa na wataalam katika kikao kazi hivho.


Meza Kuu.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni, Bw.Godfrey Nyaisa akizungumza na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw. Deodatus Balile kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah akiwasikiliza.


Naibu Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni, Bw.Godfrey Nyaisa wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa vitengo mbalimbali vya Wakala wa Usajiri wa Biashara na Leseni.


Naibu Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni, Bw.Godfrey Nyaisa wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa vitengo mbalimbali vya Wakala wa Usajiri wa Biashara na Leseni na baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.

..............................

WIZARA ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imesema kuwa, wahariri wa vyombo vya habari nchini wana nafasi kubwa kupitia vyombo vyao kufanikisha ukuaji wa sekta ya biashara nchini.

Hayo yamesemwa leo Mei 21, 2022 na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji kupitia hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Katibu Mkuu,Dkt.Hashil Abdallah katika kikao kazi cha siku mbili kati ya wahhariri wa vyombo vya habari na BRELA kinachoendelea mkoani Morogoro.

"Hivyo kwa muktadha huu niwaombe wahariri tushirikiane kwa pamoja kwenye kufanikisha ukuaji wa sekta ya biashara nchini, hasa wananchi warasimishe biashara zao. Kupitia nyie watakuwa na uelewa wa mambo mengi,"amesema Dkt.Abdalah kwa niaba ya Waziri Dkt.Kijaji.

Pia maesema, kupitia kikao kazi hicho anaamini wahariri watakuwa mabalozi wazuri wa BRELA kwa kuwa ajenda za wakala huo hususani kwenye urasimishaji wa biashara watazibeba ili wananchi waweze kupata taarifa njema ambazo zitawawezesha kunufaika kupitia wakala huo.

Katika hatua nyingine, Dkt.Abdalah amesema,BRELA wanapaswa kuendelea kuimarisha ushirikiano na vyombo vyote vya habari na kila wanapotakiwa kutoa ufafanuzi wa jambo fulani wasisite kufanya hivyo.

"BRELA, muelewe kuwa wahariri wana jukumu la kuandika habari kwa usawa, pindi wanapotaka kutoa habari kwenu msiwe wagumu kutoa taarifa, kama majibu ya maswali yao yapo kwa muda huo wapewe ili umma upate taarifa kwa haraka na kama habari wanayohitaji inachukua muda kupata majibu wapewe mrejesho mapema ili waweze kusubiri ili upotoshaji usiwepo.

"Mkumbuke kuwa, Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kila mtu-(a) ana uhuru wa kuwa na maoni na kujielekeza na kutoa maoni au mawazo yake, (b) ana haki ya kutafuta, kupokea na, au kusambaza taarifa bila kujali mipaka ya nchi,

"(c) ana uhuru wa kuwasiliana na haki ya kulindwa dhidi ya kuingiliwa kati ya mawasiliano yake, na (d) ana haki ya kupata taarifa wakatin wote kuhusu matukio mbalimbali yanayoendelea kuhusu maisha. Hivyo (BRELA), mtambue kuwa ibara hii inawalinda wahariri wa vyombo vya habari katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kutoa habari muhimu zenye maslahi kwa umma na umma pia una haki ya kupata taarifa,"amesema Dkt.Abdalah kwa niaba ya Waziri Dkt.Kijaji.

Wakati huo huo, Dkt.Abdalah amewaomba wahariri wanapotekeleza majukumu yao kutumia lugha rahisi kuwaeleza wananchi masuala ya BRELA, kwani mambo mengi ya wakala huo yapo kisheria.

"Wapo wahariri wengine wanaweza kuwa na mitazamo tofauti kwa namna wanavyotafsiri sheria za utekelezaji wa majukumu ya BRELA na kupelekea muda mwingine kuandika kichwa cha habari kinachopiga kelele au kichwa cha habari kinachohukumu na kuleta taharuki kwa umma, ninaamini kupitia mkutano huu mtajadili kwa kina yale ambayo yamekuwa yakiwatatiza na kupata majibu ya kina,"amesema Dkt.Abdalah.

Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni, Bw.Godfrey Nyaisa amesema kuwa, usimamiaji wa majukumu ya msingi ya BRELA umewezesha kuwa na mafanikio makubwa yenye uwazi na ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Bw.Nyaisa amesema kuwa, hali hiyo inatokana na uboreshaji wa mazingira ya biashara na urahisishaji wa sajili na leeni zinazotolewa na BRELA hapa nchini.

"Mafanikio haya yametokana na utekelezaji wa mikakati mikuu ya Kitaifa, Sera na Mpango wa Maendeleo ya Taifa,"amesema Bw,Nyaisa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com