Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, amewaagiza viongozi wa chama hicho wanaowania uongozi katika uchaguzi wa ndani, kukaa pembeni na wateuliwe wengine kushiriki vikao vya maamuzi.
Chongolo ametoa kauli hiyo leo, Mei 27, 2022 wakati akisalimia wana-CCM Mkoa wa Shinyanga, alipofika kwa ziara ya kikazi inayolenga kuimarisha Chama, kuwasalimu wanachama na kukagua miradi ya maendeleo.
Amesema kufanya hivyo, kutaepusha ujanja ujanja wa kunyimana fomu na kuteuliwa kwa wagombea wasio na sifa.
"Kuanzia leo nchi nzima, mahali ambapo pana kiongozi anayegombea, kiongozi huyo atakaa pembeni asishiriki kikao cha maamuzi ili awatendee haki wenziwe na wenziwe wamtendee haki yeye,” amesema.
Katibu Mkuu was CCM Ndugu Daniel Chongolo ameanza ziara ya siku 9 katika mikoa ya Shinaynga na Simiyu Kwa ajili ya kukagua uhai wa Chama hasa kipindi hiki ambacho chama kinafanya ucaguzi wa ndani lakini pia kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kupitia ilani ya uchaguzi ya 2022-2025.