Kondoo atatumikia kifungo katika kambi ya jeshi kwa miaka yote mitatu
Huko nchini Sudani Kusini, kondoo amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mwanamke mwenye umri wa miaka 45.
Kondoo huyo alikamatwa mwezi mmoja uliopita na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kumshambulia na kumjeruhi mwanamke anayefahamika kwa jina la Adhieu Chaping ambaye baadaye alifariki kwa majeraha hayo.
Mmiliki wa kondoo, Duony Manyang Dhal ameamriwa na mahakama kutoa ng'ombe watano kwa familia ya marehemu.
Social Plugin