Swalha enzi za uhai wake
Mwanaume aitwaye Said Oswayo anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi kadhaa mke wake Swalha Salum (28) mkazi wa Kirumba jijini Mwanza usiku wa Jumamosi Mei 28, 2022 amekutwa amejiua.
Wanandoa hao walifunga pingu za maisha Disemba 30, 2021.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Mairi Makori amethibitisha kujiua kwa Said Oswayo ambaye alikuwa anasakwa kwa mauaji ya mke wake na kwamba mwili wake umekutwa ndani ya Ziwa Victoria kwenye ufukwe wa Rock Beach jijini Mwanza ukiwa na majeraha ya risasi kichwani.
Kamanda Makori amesema mwili huo ulikutwa unaelea ufukweni mwa Ziwa Victoria ufukwe wa Rock Beach ambapo Jeshi la Polisi lililazimika kuwatafuta ndugu kwa utambulisho na kuthibitisha kuwa mtu huyo ndiye mtuhumiwa aliyekuwa anasakwa kwa mauaji ya mke wake.
Mdogo
wa marehemu mwenye umri wa miaka 15 amesema kabla ya tukio hilo lililotokea
usiku wa Jumamosi Mei 28, 2022 marehemu dada yake na mume wake (shemeji) Said Oswayo walikuwa na ugomvi huku sauti za majibizano zikisikika
kutoka chumbani na baadaye walibaini mwili wa dada yake ukiwa
kitandani ukivuja damu.
“Mimi
na House girl wetu tulikuwa tukiandaa chakula cha usiku. Tuliwasikia dada na shemeji wakizozana
kwa muda wa takribani nusu saa ndipo tukasikia milio ya kwanza ya risasi. Nilikimbilia
chumbani kwao na kubisha hodi lakini hakukuwa na jibu nikaamua kuondoka. Muda
mfupi baada ya milio ya kwanza ya risasi, kulisikika milio mingine na niliporejea
tena kugonga mara ya pili mlango wa chumbani,shemeji alitoka na kuniambia kuwa hakuna
tatizo niendelee tu shughuli zangu ila akasema wana mkwaruzano kidogo
kutokana na dada yangu kutopokea simu yake zaidi ya mara 37",ameeleza
mtoto huyo.
Soma Pia :
Social Plugin