Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay akiwa amebinuka sarakasi ndani ya ukumbi wa Bunge alipokuwa akichangia mjadala wa kupitia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 jijini Dodoma leo Mei 23,2022.
Flatei alichukua uamuzi huo ikiwa ni njia ya kuonyesha hisia zake kwa kero ya kutokuwa na barabara ya lami katika jimbo lake. Picha na Edwin Mjwahuzi
Flatei amesema licha ya kuahidiwa ujenzi wa barabara hiyo tangu katika bajeti ya mwaka jana, Kamati ya Bunge ya Miundombinu imeonyesha fedha zilizotengwa mwaka jana zimepelekwa kulipa madeni.
Amesema katika kitabu cha bajeti cha mwaka huu imeonyeshwa kuwa barabara hiyo itajengwa katika kiwango cha lami lakini kwa Kilometa 25.
“Kama waliniahidi kuwa barabara itajengwa hilo tangazo linachukua muda gani? Mimi hapa mheshimiwa Spika sio shilingi tu. Mimi wananchi wameniambia shilingi niichukue niende nayo Mbulu Vijijini maana hapa hamna namna tena,” amesema.
Alimhoji Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kama hamtoi nje ya ukumbi wa Bunge basi apige sarakasi.
“Mimi naona wanataka kunitengenezea ajali kuliko kukitengenezea ajali chama changu si bora uruhusu tu niruke hapa ili wastuke sasa nitafanyaje sasa,”amesema.
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI.
Social Plugin