Mwanamke mmoja huko nchini Serbia, Teresa Peric (46) amekuwa gumzo mno baada ya kutiwa mbaroni akidaiwa kumuua mumewe, Srdjan Peric (42).
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya kimataifa, Teresa alimuwekea madawa kwanza ndipo akaanza kumchomachoma mumewe huyo kwa kisu na kumkatakata nyeti kisha kupika mapande ya mwili wa mumewe zikiwemo korodani alizozikata kwa msumeno.
Binti wa mwanamke huyo amedaiwa kushuhudia kila kitu na alikwenda kumuita kaka yake, lakini na wao walianza kutishiwa na mama yao.
Kwa mujibu wa taarifa, Teresa na Peric walianza kuishi pamoja miaka miwili iliyopita na hawajazaa pamoja, lakini kila mara wamekuwa wakishushiana vipigo. Pia wote wanadaiwa kutumia madawa ya kulevya na wote wanaelezwa kuwa wana matatizo ya akili ingawa haijathibitishwa na madaktari.
Teresa alishaolewa mara nne na kila ndoa alizaa mtoto mmoja hivyo ana watoto 4 kila mmoja na baba yake.
Hivi karibuni, Teresa alidaiwa kupeleka moto kitandani alipokuwa amelala mumewe huyo kwa lengo la kumuunguza, lakini mumewe akajinasua.
Mara kwa Mara waligombana huku mke akimtuhumu mumewe huyo kuwa ni mvivu
Social Plugin