Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho kwa Naibu Makatibu Wakuu kama ifuatavyo:
- Uteuzi:
- Amemteua Dkt. Charles Enock Msonde kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI (Elimu). Bwana Msonde amechukua nafasi ya Bw. Gerald Mweli ambaye amehamishiwa Wizara ya Kilimo. Kabla ya uteuzi huu Dkt. Msonde alikuwa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).
- Amemteua Dkt. Maduhu Kazi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Dkt. Kazi amechukua nafasi ya Bwana Ramadhani Kailima aliyehamishiwa TAMISEMI. Kabla ya uteuzi huu Dkt. Kazi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC).
- Uhamisho:
- Bwana Ramadhan Kailima Kombweyi, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi amehamishwa na kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), amechukua nafasi ya Dkt. Switbert Zakaria Mkama ambaye amehamishiwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano).
- Bwana Gerald Mweli, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) amehamishwa na kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo.
- Dkt. Switbert Zakaria Mkama, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) amehamishwa na kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, amechukua nafasi ya Bwana Edward Gerald Nyamanga ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Social Plugin