Madiwani na viongozi mbalimbali waliohudhuria kikao cha Baraza la Madiwani katika ukumbi wa Manispaa ya Bukoba.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba Godson Gypson akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani
Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba Mh. Hamid Njovu akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani katika ukumbi wa Manispaa ya Bukoba
**
Na Mbuke Shilagi Kagera.
Baraza la Madiwani Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera limeazimia wagonjwa wanaolazwa katika kituo cha Afya Zamzam kutozwa elfu tatu ya kitanda kwa siku badala ya elfu 10 kama ilivyokuwa hapo awali.
Maamuzi hayo yamefikiwa kwenye katika kikao cha robo ya tatu ya mwaka ya Baraza la Madiwani wa Halimashauri ya Manispaa ya Bukoba kilicho fanyika katika ukumbi wa Manispaa Mei 18, 2022.
Akitoa taarifa juu ya maazimio hayo katika Kikao cha Baraza la Madiwani Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba Godson Gypson amesema kuwa wagonjwa wote watakao lazwa kwenye kituo hicho cha Afya kulipia elfu tatu ya kitanda kwa siku na si vinginevyo.
Ameongeza kuwa kwa wagonjwa watakao tozwa zaidi ya elfu tatu ya kitanda kwa siku kutoa taarifa katika ofisi yake au wafike katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba ili atua zichukue mkondo wake.
Naye Mganga Mkuu wa Manispaa ya Bukoba Dkt. Mustafa Waziri amesema kuwa lengo la wodi hiyo ilikuwa kwa wanao tumia Bima lakini pia wananchi wengine walitaka kulazwa katika kitio hicho hivyo wakaweka kiwango cha elfu 10 kutokana na uchache wa vitanda katika wodi hiyo kwa lengo la fedha hizo kutumika kulipia wahudumu wa usafi katika kitio hicho.
"Malalamiko yalikuwa mengi kuhusu Kituo Cha Afya kwahiyo tulichofanya tukakaa vikao na kuleta kwenye Baraza wakaidhinisha kwamba sasa bei iwe elfu tatu ya kitanda kwa siku kwa mgonjwa atakaye lazwa badala ya elfu kumi", amesema.
Ameongeza kuwa kupungua kwa bei ya kitanda kumekuwa na changamoto ya wagonjwa wengi wanao takiwa kulazwa katika kituo hicho, ambao wanazidi idadi ya vitanda vilivyomo katika wodi hiyo ikiwa idadi ya vitanda katika wodi ni jumla ya vitanda 14.
Social Plugin