Diwani wa kata ya kashai Mh. Ramadhani Kambuga akizungumza na waumini wa Dini ya kiislam katika ibada ya Eid al Fitr
Aliyesimama ni Sheikh wa Wilaya ya Bukoba Sheikh Yusuph Kakwekwe akitoa mawaidha katika ibada ya Eid al Fitr
**
Na Mbuke Shilagi Kagera.
Diwani wa kata ya Kashai Mh. Ramadhani Kambuga ameshiriki ibada ya Eid al Fitr iliyofanyika katika msikiti mpya ulio jengwa kata ya Kashai katika mtaa wa rwome Manispaa ya Bukoba ambapo ibada hiyo imeongozwa na Sheikh wa Wilaya ya Bukoba Sheikh Yusuph Kakwekwe.
Diwani Kambuga ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika ibada hiyo amewataka wananchi kudumisha Amani na upendo kwa watu wote na kwa dini zote, kuilinda Amani na kuudumisha upendo wao amabao ndo kila kitu katika maisha ya kila siku ya mwanadamu.
Amewaomba kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ambazo zimekuwa zikiendelea kutelekezwa katika kata yake na kwamba waweze kumuombea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hasan pamoja na viongozi wote kwa kazi wanazoendelea kufanya kwa ajiri ya Taifa kiujumla.
Aidha amewataka wananchi wote wa kata ya kashai kufichua waharifu waliopo Katika kata na kwamba tayari oparesheni ya kukamata waharifu katika kata take inaendelea ili kuhakikisha wahalifu wasiwepo kabisa.
"Jambazi haulizi chama wala dini yako, jambazi anatafuta mali yako, ukimficha mhalifu anaanza na wewe, hivyo msiwafiche wahalifu toeni ushirikiano ili kuwabaini wahalifu, watu mbaki salama na mali zenu",amesema Diwani Kambuga.
Social Plugin