Chama cha Waandishi wa Habari wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Tanzania (OJADACT) kwa kushirikiana na THRDC na Jeshi la Polisi Nchini kimeandaa warsha kwa njia ya mtandao ya kujadili nafasi ya vyombo vya habari kwenye kuripoti matukio ya kihalifu.
Hivi karibuni kumekuwa na matukio ya makundi ya kihalifu kuvamia mitaa na kujeruhi watu, vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele kwenye kuripoti matukio hayo, lakini pia kumekuwa na mapungufu wakati wa kuripoti matukio hayo kiasi cha kupoteza mantiki na dhana ya kuelimisha jamii kuachana na uhalifu.
Hivyo OJADACT kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na THRDC tumeandaa warsha hiyo ili tupitishane kwenye njia sahihi ya kuripoti matukio ya kihalifu na kusaidia kutoa elimu kwa jamii kutojihusisha na matukio yanayohusisha panya road.
Warsha hiyo itafanyika kesho Jumamosi Mei 14, 2022 kuanzia saa 9.00 Alasiri kwa njia ya mtandao wa zoom.
Mgeni Rasmi
IGP Simon Siro
Wazungumzaji
1.SACP. David Misime
Msemaji wa Jeshi la Polisi
2.Edwin Soko
Mwenyekiti OJADACT
3.Onesmo Olengurumwa
Mratibu THRDC
4.Christina Richard
Kaimu Mkuu Kitengo cha Mwasiliano Wizara ya Mambo ya Ndani
Link ya mkutano
Join Zoom Meeting
https://us02web.zoom.us/j/81373269711
Meeting ID: 813 7326 9711
Passcode: 570276
Muda. Saa 9 Alasiri
Mei 14.2022
Kuzuia uhalifu ni wajibu wangu, wako na wetu
Social Plugin