Rais wa Malawi Lazarus Chakwera
Jeshi la Polisi nchini Malawi linamshikilia muuguzi wa afya katika hospitali ya wilaya ya Ntcheu kwa tuhuma za kuandika maneno ya kumkashifu Rais wa nchi hiyo Lazarus Chakwera, kupitia WhatsApp 'group'.
Naibu Msemaji wa Polisi nchini humo Harry Namwaza, amesema kwamba muuguzi huyo aitwaye Chidawawa Mainje (39), alikamatwa Jumamosi na amefunguliwa mashtaka ya unyanyasaji wa mtandaoni.
Muuguzi huyo anadaiwa kumtukana Rais Chakwera, baada ya kuibuka kwa mjadala kupitia kikundi cha WhatsApp (WhatsApp group) kuhusu hali ya uchumi wa nchi hiyo na kisha kumkosoa Rais na ndipo mmoja wa mwanakikundi aliuchukua ujumbe huo na kuutuma kwa mamlaka za usalama.
Social Plugin