Waliokuwa wanachama wa Chadema, Halima Mdee na wenzake 18 wamefika kusikiliza rufaa zao katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
***
Leo Mei 11, 2022 CHADEMA wanafanya kikao cha Baraza Kuu katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam lenye ajenda tano na kuhudhuria na wajumbe zaidi ya 400 wa chama hicho, wanaotoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema Baraza Kuu litakuwa na ajenda tano ambayo ni mpango mkakati wa chama kwa miaka tano pamoja na mpango kazi wa mwaka.
Mrema amesema ajenda nyingine itakuwa ni rufaa ya nidhamu iliyokatwa na wabunge 19 wa viti maalumu wakiongozwa na Halima Mdee wakipinga kuvuliwa uanachama na kamati kuu ya chama hicho iliyoketi mwisho mwa mwaka 2020.
Kundi hilo maarufu Halima Mdee na wenzake jana walikuwa bungeni na baadhi yao walipata nafasi ya kuuliza maswali na kuchangia makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka 2022/2023.
Wabunge hao ambao hukaa mbele pembeni kushoto mwa kiti cha Spika hawakuonekana muda wote wa kipindi cha maswali na majibu na walioonekana kwa upande huo walikuwa ni wabunge wa ACT-Wazalendo ambao nao hukaa upande huo.
TAZAMA MATANGAZO LIVE HAPA
Social Plugin