Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAFANYAKAZI SUMVE WAZURU KABURI LA HAYATI MAGUFULI

Baadhi ya wafanyakazi wa shule ya sekondari ya wasichana Sumve iliyopo mkoani Mwanza, wakiwa wamezuru kaburi la Hayati Dk. Magufuli ikiwa ni kuadhimisha siku ya wafanyakazi Duniani.

**
Na Daniel Limbe, Geita
KATIKA kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani, kundi la watumushi takribani 40 wa shule ya sekondari ya wasichana Sumve iliyopo iliyopo wilayani Kwimba mkoani mwanza, wametembelea kaburi la Hayati Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Hatua hiyo imelenga kutambua mchango wake mkubwa kwa wafanyakazi nchini na kwamba jitihada na maono yake kwa wafanyakazi hayatosahaulika daima.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi, mkuu wa shule hiyo, Sister Xaveria Thomas, amesema kutokana na mafanikio makubwa ya kimaendeleo yaliyopatikana enzi za utawala wa Hayati Dk. Magufuli wamelazimika kutumia siku ya wafanyakazi duniani kutembelea kaburi lake nyumbani kwao kijiji cha Rubambangwe Mlimani wilayani Chato mkoani Geita.

"Hayati Dk. Magufuli, alikuwa mfanyakazi aliyependa na kuithamini sana kazi yake...kwahiyo kutembelea kaburi lake na kufanya ibada fupi ya maombezi kwetu wafanyakazi wa shule ya sekondari ya wasichana Sumve tunaona fahari sana",amesema.

"Ni vema serikali yetu ikayaendeleza mazuri yote yaliyoasisiwa na hayati Dk.Magufuli ikiwa ni pamoja na kukamilisha miradi iliyoachwa pamoja na kuwataka wananchi kufanya kazi kwa bidii...kwa kuwa ndiyo kipimo cha utu na mafanikio katika maendeleo"amesema Milengo.

Kwa upande wake Mwalimu Jovinus Bwire, amedai kupitia siku ya wafanyakazi duniani anajifunza uthubutu, uadilifu, upendo na imani kwa hayati Dk. Magufuli kwa kuwa enzi za uhai wake amewahi kuwa mwalimu wa shule ya sekondari Sengerema iliyopo mkoani mwanza.

"Kwa hiyo sisi walimu tunajivunia kazi yetu kupitia hayati Magufuli kwa kuwa ni moja ya walimu waliokuwa na maono makubwa kwa maendeleo ya jamii...ndiyo maana tunajivunia kutoka mwanza hadi Chato mkoani Geita",amesema Bwire.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com