Rose Jackson,Arusha
Waandishi wa habari mkoani Arusha wamepatiwa semina ya kuwajengea ufahamu wa Sheria mbalimbali ambazo zinagusa uendeshaji wa Tasnia ya habari nchini Tanzania.
Semina hiyo imeandaliwa MISA Tanzania yenye lengo la kuwajengea uwezo Wana habari kuhusu Sheria mbali mbali ambazo zimekuwa zikiminya Uhuru wa habari
Akitoa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari mwezeshaji wa mafunzo Jesse kwayu amesema lengo la semina hiyo pia ni kutoa mafunzo kuhuusiana na Uhuru wa kujielezaa kwa wanahabari hapa nchini
Amesema kulingana na katiba ya jamuhuri ya Muungano wa watazania ya mwaka 1977 ibara 18 inasema wandishi wa habari ni wawezeshaji wa umma wa kutumia haki ya kujielezaa na Uhuru wa kutoa maoni pamoja na Uhuru wa kuchakata na kusambaza habari kupitia vyombo mbali mbali vya habari na kuweza kuwafikia wananchi.
Naye mjumbe wa bodi wa MISA Tanzania Musa Juma amesema katika semina hiyo wameweza kujadili na kupata maoni ya waandishi kuhusu maboresho ya Sheria ya huduma ya habari na namna wanavyoweza kushawishi kuwepo kwa Sheria rafiki kwa wandishi wa habari.
Kwa upande wao waandishi wa habari Jamila omary aliyeshiriki semina hiyo ametoa wito kwa waandishi wa habari kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria na kuwataka kujitokeza kutoa maoni kuhusiana maboresho ya Sheria ya huduma ya habari ili waweze kufanya kazi za kiuandishi na kuelimisha jamii.
Social Plugin