Mfano wa kichaka
Na Mwandishi wetu - Iringa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa linamshikilia mwanamke mwanamke aitwaye Desderia Mbwelwe (56) kwa tuhuma za kumlazimisha kufanya mapenzi mtoto mwenye umri wa miaka nane (8) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Kamanda wa polisi mkoani Iringa ACP Allan Bukumbi amesema mwanamke huyo alifanikiwa kumkamata mwanafunzi huyo kisha kumvutia kichakani na kumlazimisha kufanya mapenzi kwa kutumia nguvu kitendo kilichopelekea maumivu makali sehemu za siri za mtoto huyo.
Amesema wanamshikilia mtuhumiwa huyo na upelelezi ukikamilika litamfikisha mahakamani.
Social Plugin