Makumbusho ya Taifa nchini imetakiwa kuongeza kasi ya kuhakikisha vituo vidogo vya Makumbusho pamoja na vya Malikale vinaongeza uzalishaji wa mapato tofauti na ilivyo sasa.
Waziri Chana ameyasema hayo alipofanya ziara ya kikazi Kijiji Cha Makumbusho na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kwa lengo la kupewa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo na kujionea shughuli mbalimbali za uhifadhi.
Akiwa Kijiji cha Makumbusho, Waziri Chana alisema licha ya kazi nzuri ya uhifadhi wa Utamaduni wa Makabila yatu pamoja na Mazingira lakini ipo haja sasa ya kuongeza ubunifu zaidi wa program zitakazo toa nafasi kwa watalii kujifunza zaidi ya nyumba zilizopo mfano kuwa na siku ya vyakula vya asili nk
"Nachua nafasi hii kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, kwa kutuonesha njia, hivyo kama Wizara tunatakiwa tuitendee haki heshma hii aliyo tupatia kupitia Filamu ya Royal Tour, ninataka kuona na ninyi Makumbusho ya Taifa mnaitendea haki heshima hii kwa kuboresha maeneo yenu ili watalii waje kujionea Urithi adhimu uliohifadhiwa hapa" Waziri Chana
Waziri Chana akiwa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, alijionea uhifadhi mkubwa wa urithi wa vielelezo vya tunu za Taifa kama vile hati ya Uhuru, Vifaa vilivyo tumika kuchangaya udogo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, fuvu la Binadamu wa kale anaesadikika kuishi liaka zaidi ya milioni 1.7 (Zinjanthropus).
Pia Waziri Chana alipata nafasi ya kuona Hifadhi kubwa ya vifaa vya Mila na desturi, matokeo ya tafiti za kibaoloji, maonesho ya Sanaa za kale na za sasa, kupewa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo pamoja na kuzungumza na watumishi.
Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo, Mkurugenzi Mkuu Wa Makumbusho ya Taifa nchini Dkt Noel Lwoga ametaja mafanikio ni pamoja na ongezeko la watalii hasa kipindi Cha UVIKO 19, mashirikiano mema na wadau mbalimbali hasa katika utafiti na program za kimakumbusho, kuandaa mpango mkakati wa Shirika 2022/2025, maboresho ya maslai ya watumishi nk
Dkt Lwoga ameongeza kuwa licha ya mafanikio yaliyopo, Taasisi hiyo inakusudia kuenedea kufanya maboresho Makubwa kwenye Makumbusho zote za Taifa pamoja na Vituo vya Malikale ili kuvutia watalii zaidi wa ndani na wakimataifa.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi (RAAWU) Tawi la Makumbusho ya Taifa Bw Anastasius Liwewa pamoja na kumpongeza Waziri Chana kwa kazi nzuri anazo fanya, alitaja moja ya siri ya mafanikio ya Makumbusho ya Taifa kwa sasa ni uongozi mzuri uliopo unao jali maslai ya watumishi hao pamoja na mkakati mzuri wa kupeleka Taasisi hiyo kwa wananchi zaidi.
Social Plugin