Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAFANYA MAZOEZI SHINYANGA 'PJFCS' WATEMBELEA KIWANDA CHA JAMBO

Wanachama wa klabu ya mazoezi Polisi Jamii Fitness Center (PJFCS) akipiga picha ya pamoja ndani ya kiwanda cha Jambo mara baada ya kumaliza ziara yao ya kutembelea kiwanda hicho na kuona uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KLABU ya mazoezi Polisi Jamii Fitness Center (PJFCS) ya mjini Shinyanga, imetembelea kiwanda cha Jambo ili kuona shughuli za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ndani ya kiwanda hicho pamoja na kuzitangaza, ikiwa ni maandalizi ya Shinyanga Madini Marathon mbio ambazo zitafanyika Agost 7 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Klabu hiyo Sadiki Kibira, akizungumza mara baada ya kumaliza kutembelea kiwanda hicho leo Mei 20,2022, amesema katika kuelekea kwenye mbio za Shinyanga Madini Marathon Agost 7, wameamua kutangaza vivutio vyote vya hapa mkoani Shinyanga, pamoja na kutangaza bidhaa za kiwanda cha Jambo.

“Klabu yetu ya mazoezi Polisi Jamii Fitness Center Agosti 7 mwaka huu tuna mashindano ya Shinyanga Madini Marathon, ambapo kutakuwa na mbio za kilomita 21, 10, 5, 2.5 na mashindano ya Baiskeli Kilomita 60,”amesema Kibira.

“Lengo la Mashindano haya ni kusaidia watoto wenye tatizo la utapiamlo, ambapo pesa tutakazo kusanya kutoka kwa wadau wetu tutanunua Tiba Lishe na kuokoa Afya za watoto hawa,”ameongeza.

Kwa upande wake Mdhibiti ubora wa vinywaji kutoka kiwanda hicho cha Jambo Leah Stephen, ambaye alikuwa mwenyeji wao, ameishukuru klabu hiyo ya mazoezi kwa kutembelea kiwandani hapo, pamoja na kutangaza bidhaa za kiwanda hicho na kuonyesha uzalendo wa kupenda vitu vya nyumbani.

Aidha, kauli mbiu ya Shinyanga Madini Marathon inasema ‘kimbia kwa Afya saidia watoto wenye utapiamlo'.
Mwenyekiti wa klabu ya mazoezi Polisi Jamii Fitness Center (PJFCS) Sadiki Kibira, akiwa na wanachama wa klabu hiyo ndani ya kiwanda cha Jambo wakiangalia uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Ziara ikiendelea ndani ya kiwanda cha Jambo.

Muonekano wa bidhaa za Juice ndani ya kiwanda cha Jambo.

Ziara ikiendelea ndani ya kiwanda cha Jambo.

Wanachama wa Klabu ya mazoezi Polisi Jamii Fitness Center (PJFCS)  wakiangalia pipi ndani ya kiwanda cha Jambo.

Wanachama wa Klabu ya mazoezi Polisi Jamii Fitness Center (PJFCS) wakipiga picha na bidhaa za Pipi ndani ya kiwanda cha Jambo.

Ziara ikiendelea ndani ya kiwanda cha Jambo.

Wanachama wa klabu ya mazoezi Polisi Jamii Fitness Center (PJFCS) wakipiga picha ya pamoja huku wakishikilia bidhaa za Biskuti ndani ya kiwanda cha Jambo.

Wanachama wa klabu ya mazoezi Polisi Jamii Fitness Center (PJFCS) wakipiga picha ya pamoja huku wakishikilia bidhaa za Biskuti ndani ya kiwanda cha Jambo.

Wanachama wa klabu ya mazoezi Polisi Jamii Fitness Center (PJFCS) wakipiga picha ya pamoja huku wakishikilia bidhaa za Juice ndani ya kiwanda cha Jambo.

Wanachama wakipiga picha ya pamoja ndani ya kiwanda cha Jambo.

Wanachama wakipiga picha ya pamoja ndani ya kiwanda cha Jambo.

Awali wanachama wa (PJFCS) wakiwa ndani ya kiwanda cha Jambo.

Awali wanachama wa (PJFCS) wakiwa ndani ya kiwanda cha Jambo kwa ajili ya kuangalia uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kiwandani hapo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com