Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Marry Makondo akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa mawakili wa serikali nchini ya uendeshwaji wa mashauri pamoja upatanishi usuluhishi kutoka katika taasisi za umma yenye lengo la kuwajengea uwezo mawakili hao yaliyofanyika jijini Arusha.
***********
Na Agness Nyamaru, Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Mary Makondo amewataka mawakili wa serikali wote nchini kuwa waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao, kufanya kazi kwa bidii, umakini na uzalendo kwani wao wanamchango mkubwa katika kumchangia uchumi wa nchi.
Ametoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo kwa mawakili wa serikali kutoka katika taasisi za umma zilipo nchini juu ya uendeshwaji wa mashauri pamoja na upatanishi usuluhishi lengo ni kutambua umuhimu wa mawakili wa serikali katika kuchangia uandaaji wa nyaraka ipasavyo katika taasisi zote za serikali,usimamizi na uendeshwaji wa mashauri yanayofunguliwa dhidi ya serikali au serikali yenyewe yakisimamiwa na wakili mkuu wa serikali.
Inaelezwa kuwa Ofisi hiyo imechangia katika uokoaji wa mapato ya serikali kwa kuisaidia kutolipa fidia ya zaidi ya trilion kumi ambazo zingelipwa na mashauri ambayo yapo ndani na nje ya nchi ambayo kutokana na migogoro mbalimbali inayoibuka katika utekelezaji wa mikataba serikali inashtakiwa na kudaiwa fidia.
"Tunatambua wajibu wa serikali ni kuwapatia watumishi wake mafunzo hivyo dhumuni la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo mawakili wa serikali wote nchini,"alisema Makondo.
Makondo alisema ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali imefungua mfumo mahususi wa kuwatambua mawakili wa serikali na wanasheria wote utawawezesha kufanya kazi kwa weledi,bidii na uzalendo katika kuijenga nchi na kuchangia katika kuokoa madai ambayo yasipoendeshwa vizuri serikali italipa fidia kubwa.
"Fesha hizo zikiokolewa zinarudishwa katika mfumo mkuu wa serikali na kutumika katika maendeleo ya nchi na huduma zake kwa ujumla kama elimu,ujenzi wa miundombinu, sekta ya afya na kuchangia katika ujenzi wa nchi yetu,"alisema Katibu Mkuu huyo.
Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Malata alisema tangu kuanzishwa kwa ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali mwaka 2018 wamefanikiwa kuokoa zaidi ya sh. Trillion 10 ambazo kama si uimara wa ofisi ya wakili mkuu wa serikali fedha hizo zingelipwa kwa watu wasio stahili.
Malata alisema katika mafanikio yao mengine wamefanikiwa kurejesha Mali za serikali zilizochikuliwa na watu ambao hawana nia njema na serikali yao,Kutatua na kupunguza mrundikano wa mashauri kwa njia ya majadiliano pamoja na kupunguza migogoro.
"Ofisi yetu imeweza kushiriki kukuza uchumi nchini Kwa kuokoa zaidi ya trillion 10,kutatua migogoro kwa wakati hasa ya haki za binadamu ndani na nje ya nchi,"alisema Mlata.
Jenipher Kaaya ni Wakili wa Serikali mwandamizi alisema mafunzo hayo yatawajengea uwezo,weledi na kijiamini katika kushindana na mawakili wenzao mahakamani endapo wakishtakiwa watakuwa na nguvu kubwa kuliko ya awali katika kuwasilisha hoja zao za kisheria.