Wahitimu 37 wa kidato cha Sita shule ya Sekondari Don Bosco Didia wakitoa burudani
Na Josephine Charles - Shinyanga
Wanafunzi wanaohitimu Elimu ya kidato cha Sita wametakiwa kutumia elimu waliyopata kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ikiwa ni pamoja na kuielimisha Jamii.
Hayo yamesemwa na Afisa Elimu ya Watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi Mkoa wa Shinyanga Mwl. Dedan William Rutazika katika mahafali ya 21 ya Kidato cha Sita shule ya Sekondari Don Bosco iliyopo Didia Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga yaliyofanyika Aprili 30,2022
Rutazika pia ameupongeza uongozi wa Shule ya Don Bosco sekondari Kwa kutoa Elimu bora na na kuibua vipaji mbalimbali vya wanafunzi.
Aidha Rutazika amesema kuwa serikali ya awamu ya sita, inatambua mchango wa Shule binafsi kwani zinasaidia katika kupunguza uhaba wa Shule nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo Fr. Felix Wagi amewashauri wahitimu kuwa na utulivu wa mwili na akili ili kufanya vizuri katika mitihani ya mwisho.
Mahafali hayo ya 21 ambayo yalikuwa na jumla ya Wahitimu 37, yamefanyika katika Ukumbi wa Shule hiyo na kutanguliwa na Ibada ya misa takatifu iliyoongozwa na Fr. Justin Leon Msaiye ambaye ni Paroko wa Parokia ya familia takatifu Kagongwa Kahama.
Mgeni Rasmi Afisa Elimu watu wazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi Mkoa wa Shinyanga Mwl. Dedan William Rutazika akizungumza kwenye mahafali hayo
Mkuu wa Shule ya Sekondari Don Bosco Didia Shinyanga Fr. Felix Wagi akizungumza katika mahafali hayo
Mgeni Rasmi katika picha ya pamoja na Wahitimu pamoja na watumishi wa Shule ya Sekondari Don Bosco Didia Shinyanga
Social Plugin