..........................................
Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege, amefanya uteuzi na mabadiliko ya vituo vya kazi kwa Warajis Wasaidizi sita (6) ambapo Warajis Wasaidizi wa Vyama vya Ushirika watano (5) wa Mikoa na mmoja kutoka Makao Makuu ya Tume wamepangiwa vituo vipya vya kazi.
Waliohamishwa ni pamoja na: Augustino Semkuruto aliyekuwa Makao Makuu ya Tume, ambaye amehamishiwa mkoa wa Iringa kuwa Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika wa mkoa huo; Robert George, aliyekuwa Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Iringa amehamishiwa mkoa wa Kagera kuendelea na wadhifa wake; Godfrey Mpepo, aliyekuwa Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Kagera amehamishiwa mkoa wa Simiyu kuendelea na wadhifa wake.
Wengine waliohamishwa ni: Ibrahim Kadudu, aliyekuwa Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Simiyu ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Tume kuendelea na wadhifa wake; Juma M. Juma, aliyekuwa Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Katavi amehamishiwa Makao Makuu ya Tume na kuteuliwa kukaimu nafasi ya Mkurungenzi wa Mafunzo na Utafiti; na Consolata Kiluma, aliyekuwa Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Lindi amehamishiwa Makao Makuu ya Tume kukaimu nafasi ya Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika – Uhamasishaji na Uratibu.
Aidha, katika mabadiliko hayo, Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania amewateua watumishi wafuatao kuwa Kaimu Warajis Wasaidizi wa Vyama vya Ushirika wa mikoa: Peter Nyakunga, Afisa Ushirika Mkuu – Mvomero DC ameteuliwa kukaimu nafasi ya Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Katavi; Cesilia Filimin, Afisa Ushirika Mwandamizi – Mafinga TC ameteuliwa kukaimu nafasi ya Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Lindi; na Peja Mhoja, Afisa Ushirika Mwandamizi – Iringa MC ameteuliwa kukaimu nafasi ya Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Ruvuma.
Katika hatua nyingine, Mrajis amewahamisha Maafisa Ushirika wote wa Mkoa wa Kagera walioko chini ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika na kuwapangia vituo vingine vya kazi ili kuimarisha utendaji na usimamizi wa Vyama vya Ushirika katika mkoa huo. Aidha, nafasi za watumishi waliohamishwa zimejazwa na Maafisa Ushirika kutoka mikoa mingine nchini.