KIJANA mwenye umri wa miaka 18, amevamia shule ya Texas Elementary School akiwa na bunduki na kuanza kufyatua risasi ambapo wanafunzi 19 wameuawa huku watu wengine kadhaa wakijeruhiwa, wakiwemo watu wengine wawili.
Polisi wa Texas wamemtambua muuaji huyo kwa jina la Salvador Ramos kutoka Mji wa Uvalde ambaye inaelezwa kuwa kabla ya tukio hilo, alimpiga risasi bibi yake na kumjeruhi vibaya kasha akaondoka na gari na kwenda kuligongesha jirani na shule hiyo kisha kufanya mauaji hayo.
Mbali na kuuawa kwa watoto wadogo kumi na tisa, watu wazima wawili wameuawa akiwemo mwalimu Mireles, mwalimu ambaye aliripotiwa kuuawa, alikuwa na umri wa miaka 40 na alikuwa na binti chuoni, kulingana na ukurasa wake kwenye tovuti ya shule.
Alikuwa mwalimu kwa miaka 17. Ukurasa huo ulimnukuu akisema: “Ninapenda kukimbia, kupanda milima, na sasa unaweza kuniona nikiendesha baiskeli!!”
Shangazi yake, Lydia Martinez Delgado, aliambia New York Times mpwa wake “alipendwa sana” na “alikuwa mtu wa kufurahisha katika sherehe”.
Social Plugin