Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akizungumza katika kikao chake na watumishi wa sekta ya ardhi mkoani Mbeya.
Sehemu ya watumishi wa sekta ya ardhi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete (Hayupo pichani) wakati wa kikao chake na watumishi wa sekta hiyo mkoani Mbeya.
Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mbeya Siyabumi Mwaipopo akizungumza wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete na watumishi wa sekta ya ardhi mkoa wa Mbeya.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Zakariyya Kerra (Kulia) akiandika maelezo wakati wa kikao kati ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete na watumishi wa sekta ya ardhi mkoa wa Mbeya.
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dkt Rashid Chuwachuwa akizungumza katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete na watumishi wa Sekta ya Ardhi mkoa wa Mbeya
…………………………………………………..
Na Munir Shemweta na Anthony Ishengoma, WANMM MBEYA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete amewataka watumishi wa sekta ya ardhi nchini kuhakikisha wanatoa haki wakati wa kutekeleza majukumu yao kwa wananchi.
Alisema, utoaji haki uko katika sura tofauti kuanzia zoezi la utoaji hati, upatikanaji haki katika mabaraza ya ardhi na nyumba sambamba na utoaji taarifa na uwezeshaji wananchi katika ardhi au rasilimali ardhi.
Alisema, baadhi ya watendaji wa sekta ya ardhi wamekuwa miungu watu kwenye maeneo yao kuliko hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ardhi yote iko chini ya mamlaka yake na kubainisha kuwa, mwananchi anaweza kwenda ofisi ya ardhi kwa ajili ya kumilikishwa ardhi lakini adha anayoipata wakati wa kuomba kupata uhalali wa kumiliki ardhi yake basi maafisa ardhi wamekuwa wakijizungusha bila kumsaidia.
‘’kama nilivyokwisha sema yaliyopita si ndwele tugange yajayo, uabaishaji ufike mwisho tumeelewana ndugu zangu’’ alisema Rdhiwani.
Naibu Waziri Kikwete alieleza hayo tarehe 13 Mei 2022 alipokutana na watumishi wa Sekta ya Ardhi Mkoa wa Mbeya ambapo alioneshwa kutoridhishwa na utendaji kazi wa baadhi ya watumishi wasiowaadilifu.
‘’Kama kuna mtumishi anadhani kuna suala la kula kula ovyo kwenye Wizara hii ya ardhi basi siyo kwa nyakati hizi, ndugu zangu watendaji wenzangu naomba tuwe waadilifu katika kutenda haki kwa wananchi.’’ Alionya Ridhiwani Kikwete Naibu Waziri Wizara ya Ardhi.
Sambamba na hilo aliwataka Maafisa Mipango miji wa Mkoa wa Mbeya kuwa na mipango bora ya mipango miji ili jiji Mbeya lisiendelea kuwa jiji la makazi holela.
Kwa mujibu wa Ridhiwani, ukiwa kwenye ndege unaona milima ya mbeya imejengwa majengo kwenye ardhi isiyopimwa ambapo aliwataka Maafisa Mipango Miji hao kutosubiri watu kuendeleza makazi holela na baadae kujitokeza kurasimisha maeneo hayo.
‘’Acheni kusubiri wananchi wajenge alafu nyie muwafuate kuendeleza mipango miji badala yake muwe wa kwanza kupima na kupanga miji ili wanachi waishi kwenye makazi bora tofauti na sasa mnapowaa na kusababisha kuaribu milima na taswira ya jiji la Mbeya’’ alisema Ridhiwani.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete yuko mkoani Mbeya kwa ziara ya siku mbili ambako mbali na na kufanya kikao na watumishi wa sekta ya ardhi ameshiriki zoezi la utoaji hati na leseni za makazi kwa wananchi wa halmashauri ya jiji la Mbeya pamoja na wale wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mbalizi.
Social Plugin