Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NMB KUWASAIDIA WAJASIRIAMALI NA KAMPENI MPYA YA TELEZA KIDIGITALI

Afisa Mkuu wa Biashara na wateja binafsi Filbert Mponzi kutoka NMB Benki akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya teleza kidijitali,uliofanyika katika soko la Kilombero mkoani Arusha.


************


Na Agness Nyamaru, Arusha.


Taasisi ya kifedha ya NMB imezindua kampeni ya teleza kidigitali yenye lengo la kuwafanya watanzania wengi hasa wajasiliamali katika kukuza uchumi wao.

Kupitia uzinduzi wa kampeni hiyo iliyozinduliwa katika soko la Kilombero mkoani Arusha na Afisa mkuu wa biashara na wateja binafsi kutoka katika taasisi hiyo, Filbert Mponzi amesema watanzania wengi wataingia kwenye mfumo wa kibenki kwa kuwafungulia akaunti sambamba na kupata huduma za kibenki kwa njia ya kidigitali.

"Kupitia kampeni hii wananchi hawatakuwa na ulazima wa kwenda katika matawi yetu ili kufanya miamala yao kwa kupitia mishiko faster ambao ni mkopo kwa ajili ya wateja wadogo wadogo ambayo inapatikana kupitia huduma ya NMB mkononi,"alisema Mponzi.

Akielezea kampeni hiyo alisema mteja atafungua na kutokana na miamala yake ataweza kujipatia mikopo ambayo haina dhamana, mikopo midogo midogo Hadi ya sh. laki tano,ikiwa mkopo huo utawasaidia wajasiriamali wengi kama kianzio cha biashara kwa kuchukua asubuhi kwenda kujumua bidhaa anayoitaka na kuiuza na jioni kurudisha.

Mponzi alisema wateja wao wanawaletea kabisa mawakala wa NMB pesa ambao watakuwa kila sehemu ikiwa kwa kupitia mawakala hao wafanyabiashara wataweza kwenda kuweka pesa zao kwa urahisi zaidi badala ya kwenda kwenye matawi.

Aidha kwa wale wenye sehemu zao za biashara wamekuja na huduma ya lipa kwa bili (mkononi),ikiwa huduma hiyo ya kidigitali itamuwezesha majasiliamari aweze kulipa pesa zake za mauzo Kwa kupitia huduma hiyo ya kidigitali itawawezesha wajasiriamali waweze kulipa pesa zile za mauzo kwa kupitia huduma ya lipa kwa mkononi.

Afisa huyo alisema lengo kubwa ni kuhitaji watanzania wengi waingie kwenye mfumo wa kibenki na kufaidika na huduma zilizopo ikiwemo za mikopo na miamala mingine ya kibenki.

Mponzi alisisitiza kuwa huduma hiyo ipo nchi nzima ikiwa walishaanza kwa baadhi ya mikoa huku matarajio yao ni kufikia nchi nzima ili wateja waweze kufurahia huduma zao za kibenki.

Nae mmoja wa wafanyabiashara Ally Shabani katika soko la Kilombero mkoani Arusha alisema anafaidika na huduma za kibenki katika taasisi hiyo ya kifedha kwani inawasaidia wateja Kwa kuwafungulia malengo yao na kuhakikisha wanainuka kiuchumi.

"Nimeifurahia huduma hii mpya iliyozinduliwa na NMB kwa sababu wafanyabiashara wadogo wadogo tutaweza kukopa fedha asubuhi kununulia mizigo na kurudisha jioni kupitia simu,"alisema Shabani.

Angela Mboya ni mmama katika soko hilo alisema amefurahishwa na benki hiyo juu ya kampeni yao kwani inawatia chini kwenda juu kwa kuwakwamua katika changamoto zao za kibiashara wanazokutana nazo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com