Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa THRDC Jaji Mstaafu Joaquine De Mello kutokana na mchango wake wa kulinda na kusimamia haki za binadamu na utawala wa Sheria katika kipindi cha mwaka mmoja tangu aingie madarakani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akinyanyua Tuzo aliyopewa na Kituo cha THRDC kutokana na mchango wake wa kutetea Haki za Binadamu na utawala wa Sheria katika Maadhimisho hayo ya miaka 10 ya Kituo Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Mei 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wadau mbalimbali kwenye Maadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDC katika hafla iliyofanyika ukumbi wa PSSSF Jijini Dar Es Salaam tarehe 13 Mei 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua Ripoti ya miaka 10 ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDC mara baada ya hotuba yake tarehe 13 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro, Mwenyekiti wa THRDC Jaji Mstaafu Joaquine De Mello pamoja na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya THRDC mara baada ya hotuba yake tarehe 13 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kazi mbalimbali zinazofanywa na THRDC pamoja na Asasi nyingine katika mabanda ya Maonesho wakati akiwasili kwa ajili ya Maadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao huo wa Haki za Binadamu Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Mei 2022.
***
Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka watetezi wa haki za binadamu kufanya kazi za uwanaharakati zenye tija na kuibua changamoto na sio kupambana na serikali.
Rais Samia ameyasema hayo wakati akizindua ripoti ya miaka kumi ya mtandao wa watetezi wa haki za binadamu THRDC akisema kuwa wasifanye kazi kwa kupambana na serikali ila wanachopaswa kufanya ni kuikosoa serikali kwenye mapungufu ili iyafanyie kazi.
Amesema hakuna atakaejenga hii nchi bali na kila mtu ambaye ni mtanzania mwenyewe kwa ushirikiano wa pamoja kati ya serikali na wadau wake wakiwemo THRDC huku akiwakaribisha kuzngumza na serikali muda wote bila woga wowote.
“Tufanye kazi kwa pamoja tusiwe wagomvi kila kitu tuwekane wazi ninyi huko kila kitu mmekikumbatia wenye hata waziri hapa hana leteni tusome tuone nini mnacho huko na sisi tujue”.
Pia amewataka watetezi wa haki za binadamu kuaminiana serikali kwa kila mmoja kuzungumza huku akiwapongeza kwa hatua waliyoifikia kwa miaka kumi na kila mmoja andelee kufanya kazi kwa nafasi yake.
Hata hivyo Rais Samia amewahakikishia kuwapatia maeneo ya kujenga ofisi zao THRDC kama walivyoomba kwenye ripoti yao huku akiendelea kusisitiza ushirikiano wa kufanya kazi pamoja.
Social Plugin