Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt.Herbert Makoye alipokuwa akizungunza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu kampeni ya Sanaa ya maigizo kutoa elimu ya afya ya uzazi hasa madhara ya mimba za utotoni wakishirikiana na Taasisi ya Bagamoyo Friendship Society ya Ujerumani.
******
TAASISI ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa kushirikiana na Taasisi ya Bagamoyo Friendship Society ya Ujerumani imetumia Sanaa ya maigizo kutoa elimu ya afya ya uzazi hasa madhara ya mimba za utotoni.
Akizungumza wakati wa kampeni hiyo ya uelimishaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt.Herbert Makoye amesema wamejipanga kufikia takribani kata 11 zilizopo wilayani Bagamoyo na baadae wataifikia jamii nzima kwa ujumla.
Amefafanua kwamba muitikio wa utoaji wa elimu hiyo umekuwa mkubwa kwani kumekuwa na ushirikishwaji wa jamii kwa kuuliza maswali pamoja na kutoa maoni yao kuhusu masuala ya afya ya uzazi hususan madhara ya mimba za utotoni.
Pia Dk.Makoye amesema kutokana na Serikali kutoa maelekezo kuwa wanafunzi waliopata ujauzito kwa bahati mbaya waweze kurudi shuleni, sasa wameona kuna umuhimu jamii ielimishwe kuhusu suala hili kwa maana baadhi ya watu katika jamii wamekuwa na imani potofu kwenye suala hili.
"Tumeona tuchukue hatua kueleimisha jamii kwamba hili suala ni lakawaida kwahiyo waweze kuwasaidia hawa vijana ambao kwa bahati mbaya walipata ujauzito basi waweze kurudi shuleni na wapewe msaada unaotakiwa kuanzia kwenye familia zao, kwenye jamii kwa ujumla pamoja na kwenye shule wanazokwenda kusoma," amesema
Kwa upande wake Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Wilaya ya Bagamoyo Magreth Joseph amewataka wananchi kuunga mkono tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa wasichana waliokua shule mara watakapojifungua warudi shule kumalizia masomo yao kwa kuwa kila mmoja ana ndoto hivyo tuwasaidie wafikie ndoto zao.
Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Wilaya ya Bagamoyo Magreth Joseph akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu kuwataka wananchi kuunga mkono tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa wasichana waliokua shule mara watakapojifungua warudi shule kumalizia masomo yao.
Baadhi ya Wadau (waratibu wa kampeni hiyo) wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa kampeni ya Sanaa ya maigizo iliyohusu utoaji elimu ya afya ya uzazi na madhara ya mimba za utotoni iliyofanyika kwenye shule ya msingi ya Kilomo,wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.Picha zote na Michuzi JR-MMG.
Picha mbalimbali za Kikundi cha sanaa ya Uigizaji na Ngoma kutoka TaSUBa wakitoa kampeni ya Sanaa ya maigizo kutoa elimu ya afya ya uzazi hasa madhara ya mimba za utotoni wakishirikiana na Taasisi ya Bagamoyo Friendship Society ya Ujerumani
Social Plugin