Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 Blog-DODOMA
SERIKALI imesema itaanza kununua magari ya wafungwa kwa ajili ya kubeba na kuwapeleka mahakamani kutokana na magari yaliyokuwepo kuchoka na mengine kuharibika.
Hayo yalibainishwa leo Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa makambako Deo Sanga (CCM).
Amesema katika bajeji ya mwaka huu wa fedha haitaweza kumaliza changamoto ya magari hayo lakibni serikali itaendelea kununua kutokana na upatikanaji wa fedha.
”Ni kweli kwamba katika maeneo mengi magari yamechakaa na kama mtakumbuka kwa mwaka huu bajeti imeongezeka haitaweza kumaliza tatizo la uchakavu wa magari hayo lakini tutaanza kununua kutokana na bajeti ya fedha,”amesema
Aidha Mbunge huyo alihoji kuwa ni lini serikali itafanya utaratibu wa kukarabati au kuyabadilisha magari ya kupeleka na kurudisha wafungwa mahakamani kutokana na uchakavu.