Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KUANZA KUNUNUA MAGARI YA WAFUNGWA

 

Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Jumanne Sagini akiongea leo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu.

Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 Blog-DODOMA

SERIKALI imesema itaanza kununua magari ya wafungwa kwa ajili ya kubeba na kuwapeleka  mahakamani kutokana na magari  yaliyokuwepo kuchoka na mengine kuharibika.

Hayo yalibainishwa leo Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini  wakati akijibu swali la nyongeza la  Mbunge wa makambako Deo Sanga (CCM).

Amesema katika bajeji ya mwaka huu wa fedha haitaweza kumaliza changamoto ya magari hayo lakibni serikali itaendelea kununua kutokana na upatikanaji wa fedha.

”Ni kweli kwamba katika maeneo mengi magari yamechakaa na kama mtakumbuka kwa mwaka huu bajeti imeongezeka haitaweza kumaliza tatizo la uchakavu wa magari hayo lakini tutaanza kununua kutokana na bajeti ya fedha,”amesema

Aidha Mbunge huyo alihoji kuwa ni lini serikali itafanya utaratibu wa kukarabati au  kuyabadilisha magari ya kupeleka na kurudisha wafungwa mahakamani kutokana na uchakavu.

 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com