***************
NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Simba imeshindwa kufurukuta mbele ya Geita Gold Fc mara baada ya kulazimisha sare ya 1-1 kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba Mwanza.
George Mpole ameendelea kuwa mwiba kwa timu pinzani mara baada ya leo kupachika bao kwenye mchezo huo na kuendelea kufukuziana na Fiston Mayele katika kinyang'anyiro cha mfungaji bora wa ligi.
Simba Sc imeirahisishia Yanga Sc katika mbio za ubingwa ambao mpaka sasa Yanga Sc inahitaji pointi 4 tu itangazwe bingwa kwenye ligi ya NBC.
Bao la Simba Sc limewekwa kimyani na Kibu Dennis naye akiwa ana wakati mzuri katika mechi tano za hivi karibuni.
Social Plugin