Afisa Udhibiti Ubora (TBS) Bw. Isack James akifanya ukaguzi wa awali kwenye gari linalotumia mionzi ya jua sambamba na kutoa ushauri kuendana na kiwango ili likikamilika liwe bora na salama kwa matumizi. Gari hilo limetengenezwa kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo kwa ajili ya kubeba mizigo myepesi ndani ya eneo la shule na wanafunzi wa kidato cha tano kutoka shule ya sekondari Arusha Science iliyopo kata ya Lorai mkoani Arusha.
***************************
Wanafunzi wanaosoma kidato cha tano katika shule ya Sekondari Arusha Science iliyopo kata ya Laroi mkoani Arusha wametengeneza gari linalotumia mwanga wa jua (sola) ikiwa ni utekelezaji wa mafunzo kwa vitendo ambayo wamekuwa wakifundishwa shuleni hapo.
Gari hilo ambalo linatumia mwanga wa jua lina uwezo wa kutembea kilometa 160 likiwa na mzigo mwepesi baada ya hapo linahitaji kuchajiwa tena na tayari limeshatumia Sh3.5 milioni katika utengenezaji wake.