UMMY NDERIANANGA AFANYA ZIARA MKOANI TANGA NA KUTEMBELA MRADI WA TIMIZA MALENGO

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Uratibu, Sera na Bunge Mhe Ummy Nderiananga akisisitiza jambo wakati anazungumza na watendaji wa Mkoa na Tanga (hawapo katika picha) wakati wa ziara yake ya Siku moja Mkoani Tanga Tarehe 28 Mei,2022 yenye lengo la kufuatilia Progaramu ya Timiza Malengo inayolenga kuwafikia wasichana balehe na wanawake vijana wanaotokea katika mazingira hatarishi ya kupata maambukizi mapya ya VVU.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu, sera na Bunge Bw.Kaspar Mmuya akizungumza na wananchi walioshiriki katika ziara Ufatiliaji wa Mradi wa Timiza lengo Mkaoni Tanga umuhimu wa kuwashirikisha Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU (NACOPHA) pindi miradi ya kutekeleza afua za UKIMWI inapopatikana,kilia kwake ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Uratibu, Sera na Bunge Mhe Ummy Nderiananga,akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Hashimu Mgandila kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Bw.Jumanne Isango

Kaimu MKurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Bw.Jumanne Issango akizungumza na wananchi walioshiriki katika kikao cha Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu ,Sera na Bunge alipotembelea Mkoani Tanga Kufuatilia utekelezaji wa Mradi ya Timiza Malengo.

**************************

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Uratibu, Sera na Bunge Mhe Ummy Nderiananga amefanya ziara Mkoani Tanga kutembelea Mradi wa Timiza Malengo wenye lengo la kuwafikia wasichana balehe na wanawake vijana wanaotokea katika mazingira hatarishi ya kupata maambukizi mapya ya VVU.

Akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Tanga baada ya kutembelea shule ya Sekondari Nguvu mali na shule ya Msingi Majani Mapana, Mhe Ummy alisema kuwa mradi huo unawalenga wasichana walio ndani ya shule na nje ya shule, ambapo afua zinazotekelezwa kulingana na makundi yao.

“vijana walio mashuleni wanapewa elimu ya afya ya uzazi na kujikinga na VVU kupitia mashuleni na walio nje ya shule wanapewa afua zao ambazo zinazoweza kuwasaidia kubaki salama na kujiboresha kiuchumi” alisema Mhe Ummy .

Alifafanua kuwa serikali ya awamu ya sita inayogozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassani hataki kuona mtoto wa kike anashindwa kufikia ndoto zake,ndio maana,Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia TACAIDS wameona umuhimu wa kuratibu mradi huo kwa kushirikisha walimu ambao tayari wameisha elimishwa namna ya kuwafundisha vijana hao waliopo mashuleni, lakini pia hata walimu ambao hawakuweza kushiriki mafunzo hayo kujengewa uelewa na walimu walioshiriki katika mafunzo lengo ni elimu hiyo kuwafikia vijana wote kwa urahisi.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji Meneja Mradi wa Timiza Malengo Bi Maricella Kawago alisema mradi huu umeibua waelimisha rika kutoka Kata 27 za Jiji na kuwapatia mafunzo maalum kwa ajili ya kuwafikia mabinti wenzao walio katika hatari ya kupata maambukizi ya VVU na UKIMWI walio nje ya Mfumo wa Elimu kupitia program ya TASAF III na nje ya TASAF na kuwawezesha Taulo za kike.



Alifafanua kuwa Mradi wa Timiza Malengo unatekelezwa kwa miaka

mitatu (2021-2023) katika mikoa mitano ya Dodoma, Geita, Morogoro, Singida na Tanga. Ambapo katika mikoa hiyo mradi unatekelezwa katika Halmashauri 18 ambazoni Bahi, Chamwino , Kongwa , Mpwapwa, Kondoa Mji, Kondoa,Dodoma Jiji, Morogoro , Ifakara ,Malinyi,Mlimba,Geita,Chato ,Singida Manispaa, Singida , Ulanga, Tanga Jiji.



“Utekelezaji wa Mradi wa Timiza Malengo, shirika la Amref kwa

kushirikiana na Halmashauri ya Tanga Jiji linawafikia Wasichana Balehe na

Wanawake Vijana (10-24) waliopo ndani na nje ya shule”

Alifafanua kuwa afua zilizozilizotekelezwa ni pamoja na Afua za kitabibu, Huduma Rafiki za VVU na UKIMWI,Uzazi wa mpango, uchunguzi wa magonjwa ya ngono, elimu na taarifa muhimu za afya, Afua za Mawasiliano ya mabidiliko ya Tabia, Elimu ya Afya ya uzazi, elimu ya matumizi sahihi na endelevu ya kondomu na ugawaji wa kondomu, elimu rika katika vikundi na elimu ya umuhimu wa kupima VVU. Afua za kimiundombinu Uwezeshaji kiuchumi, ugawaji wa Sodo (taulo za kike) mashuleni, msaada wa kuripoti na kudhibiti ukatili wa kijinsia.

Baadae Mhe. Ummy alitembelea vikundi vya WAVIU na kuona kazi zao wanazozifanya ambazo zinawaongezea kipato ambapo walimwenza kuwa

Aidha aliagiza Halimashauri za Wilaya kuona umuhimu wa kutenga fedha za mapambano dhidi ya Virus vya UKIMWI na kwamba hatua hiyo itasaidia kuwawezesha katika miradi ya vikundi vya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (WAVIU) kufanya shughuli zao za maendeleo vizuri.

Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu, sera na Bunge Bw.Kaspar Mmuya amesema Baraza watu wanaoishi na VVU ambao wamejitokeza na kujitangaza na kusema wako tayari kushirikiana na serikali kutoa elimu (NACOPHA) ni baraza muhimu.

“ Baraza la watu wanaoishi na VVU ni muhimu kwakuwa wamekuwa msaada sana hata kushawishi na kurejesha WAVIU wengine walioacha kutumia dawa kwa sababu mbalimbali”.

Ni muhimu miradi yote inayokuja na inahusu Mwitikio wa UKIMWI Baraza la watu wanaoishi na VVU (NACOPHA) lishirikishwe kwakuwa kazi wanayoifanya ni kubwa sana.

Awali Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Afya Mkoa wa Tanga Dkt.Clemence Marcell alisema kuwa Maambukizi ya VVU yamepungua kutoka asilimia 3.5 mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 3.2. kwa mwaka 2021.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Bw.Jumanne Issango ameshukuru jitihada zinazotekelezwa na Mkoa wa Tanga katika kuhakikisha Maambukizi yanapungua lakini kwa ushirikiano wanaouonesha katika afua zinazotekelezwa na Programu ya Timiza Malengo.

“Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania ni Mratibu wa mwitikio wa UKIMWI nchini,ambapo wajibu wake pia ni kuhakikisha raslimali za kutekeleza afua za mwitikio wa UKIMWI zinapatikana ,sisi tunaendelea kwa kushirikiana na wadau kutekeleza wajibu wetu lakini pia suala la UKIMWI sio la Mtu mmoja hivyo ushirikiano wetu utafanya tufikie mlengo ya kumaliza UKIMWI ifikapo 2030”.alisema Bw.Issango.

wanasaidia hata kutafuta watu wengine ambao wemeacha kutumia dawa kutokana na sababu mbalimbali ni raslimali kubwa sana kufikia malengo yetu, kuwa serikali imetoa sh bilioni moja kwa ajili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post