Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WADAU WA FILAMU DODOMA WAPIGWA MSASA NA BODI YA FILAMU


Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt. Kiagho Kilonzo akifungua Mafunzo ya Filamu kwa Wadau wa Filamu yaliyoandaliwa na Bodi kwa lengo la kuwajengea uwezo Wadau, Jijini Dodoma


Mkurugenzi Msaidizi Haki na Maendeleo ya Wasanii kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Asha Salim Mshana akisisitiza mbinu bora za kuzingatia katika utayarishaji wa Filamu wakati wa Mafunzo ya Filamu.


Muwezeshaji Bw. Sikalion Rwabona kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) akifafanua jambo wakati wa Mafunzo ya Filamu kwa Wadau wa Filamu


SEHEMU ya Wadau wa Filamu wakifatilia mada mbalimbali wakati wa Mafunzo ya Filamu kwa Wadau wa Filamu yaliyotolewa leo jijini Dodoma.

...................................................

Bodi ya Filamu Tanzania katika jitihada za kuhakikisha kuwa Wadau wa Filamu wanaongeza ubora katika utayarishaji wa Filamu zinazokubalika Kitaifa na Kimataifa kwa lengo la kukuza masoko ya Filamu imezindua mafunzo kwa Wadau wa Filamu jijini Dodoma Mei 26,2022.

Akifungua mafunzo hayo Katibu Mtendaji wa Bodi Dkt. Kiagho Kilonzo amewataka Wadau wa Filamu kutumia fursa hiyo kujiongezea maarifa mbalimbali kupitia mada zitakazotolewa sambamba na mafunzo kwa vitendo yanayoendelea. Akieleza ni matarajio ya Bodi kuwa mafunzo hayo ni muhimu katika kuwaanda wataalamu watakatoa Filamu bora zitakazochangia kuongeza ajira na kipato kwa Wadau wa Filamu na Uchumi.

Aidha, ilibainishwa kuwa baadhi ya mada zitakazokuwa katika mafunzo hayo ni pamoja na masuala ya uandishi wa miswaada, upigaji picha, uhariri na uongozaji wa Filamu. Wawezeshaji katika Mafunzo hayo ni pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Haki na Maendeleo ya Wasanii kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Asha Salim Mshana, Bw. Sikalion Rwabona kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na Bw. Ally Makata kutoka Bodi ya Filamu.

Washiriki wa Mafunzo hayo ni Wadau mbalimbali wa Filamu wa Jiji la Dodoma wakiwemo Wapiga Picha, Waigizaji, Wahariri, Waongozaji, Waandishi wa Miswaada. Mafunzo hayo yanatarajia kufikia Tamati Mei 30, 2022 Jijini Dodoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com