Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI BASHUNGWA AKABIDHI VITENDEA KAZI VYA ELIMU


Waziri wa TAMISEMI Inncent Bashungwa (Kulia) akimkbidhi Naibu katibu mkuu anayeshughulikia elimu Dkt. Charles Msonde (Kushoto)moja ya vitendea kazi vya elimu na kusisitiza uwajibikaji wa majukumu kwa kufuata miongozo, sheria na taratibu za Serikali.


Na Dotto Kwilasa,DODOMA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent  Bashungwa  amewakabidhi vitendea kazi Naibu Katibu Mkuu - TAMISEMI  Ramadhan Kailima na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo tarehe 23 Mei 2022 katika Ofisi  ya Rais -TAMISEMI yakishuhudiwa  na Menejiment ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi hiyo.

Waziri Bashungwa amewakaribisha viongozi hao na kusema  wamekuja kwenye Treni iliyoko kwenye mwendokasi hivyo wanapaswa kudandia  na kuendelea na safari.

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Ramadhan Kailima amesema  kuziimarisha Sekretarieti za Mikoa kutasaidia kuimarisha usimamizi wa majukumu ya Halmashauri hivyo ameahidi kusimamia eneo hilo kikamifu ili waweze kufanyaka kazi kwa kufuata miongozo, sheria na taratibu za Serikali.

Naye Naibu Katibu Mkuu Elimu Dkt.Charles  Msonde amewataka watumishi wa Ofisi ya Rais Tamisemi kufanyakazi kwa ushirikiano ilikuleta matokeo chanya katika Sekta ya Elimu hasa elimumsingi na kuaihidi kuendelea kuimarisha elimu nchini.

“Nimefurahi kuletwa sehemu ambayo viongozi wake wote tunafahamiana na tumefanya kazi kwa muda mrefu kwa umoja huu naamini tutaleta mabadiliko  katika sekta ya elimu  nchini”, amesema  Dkt. Msonde 

Kwa upande wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Elimu Gerald Mweli ambaye sasa amehamishiwa Wizara ya Kilimo ameushukuru uongozi wa TAMISEMI  na watendaji wake kwa kufanya kazi kwa ushirikiano kwa wakati wote aliokuwepo Ofisi ya Rais - TAMISEMI.

“Mafanikio yoyote yale huletwa kwa ushirikiano ninawashukuru sana viongozi na watendaji wote katika Sekretarieti  za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Maafisa Elimu Mikoa na Halmashauri nchini na niwaombe tuendelee kufanya kazi kwa bidii kwa maendeleo ya nchi”, amesema Mweli.

Katika Mabadiliko yaliyofanywa hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alimhamishia Bw. Ramadhan Kailima kuwa Naibu Katibu Mkuu-TAMISEMI kuchukua nafasi ya Dkt.Switbert Mkama ambaye alihamishiwa Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira. 

Pia alimteua Dkt. Charles Msonde kuwa Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia (Elimu)  kuchukua nafasi ya Gerald Mweli ambaye amehamishiwa Wizara ya Kilimo kuwa Naibu Katibu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com